Vigogo Ahly katika kiti moto Afrika

Johannesburg, Afrika Kusini (AFP)
Al Ahly, ambayo inashikilia rekodi ya kutwaa ubingwa wa soka Afrika mara tisa, inakabiliana na hali ngumu isiyotarajiwa katika kampeni yake ya Ligi ya Mabingwa wakati itakapoikaribisha A.S Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwishoni mwa wiki hii.
Kipigo cha ugenini walichopewa na Simba ya Tanzania kimeifanya klabu hiyo ya jijini Cairo kuwa katika nafasi ya tatu ya Kundi A baada ya mechi za raundi mbili za Ligi ya Mabingwa.
Hali kadhalika, kocha Pitso Mosimane ambaye yuko katika kiti moto, aliiangalia Ahly kwa makini wakati ilipopata ushindi usioridhisha wa mabao 2-1 dhidi ya timu iliyo chini ya msimamo wa Ligi Kuu ya Misri, El Gaish, kipigo kilichozidisha kelele za kukosoa nyota wake.
Ahly ilitangulia kuruhusu bao kabla ya kusawazisha na baadaye kupata bao la ushindi katika muda wa majeruhi, bao lililofungwa na Mnigeria Junior Ajayi, mmoja wa wachezaji watano ambao si raia wa Misri wanaopangwa na Mosimane.

Upangaji viungo wasioshambulia
Mchambuzi wa soka katika televisheni na nyota wa zamani wa Ahly, Wael Gomaa alimlaumu Mosimane baada ya timu hiyo kupoteza mchezo wa Dar es Salaam, akisema "hana ujasiri wa kuingiza wachezaji was akiba wenye akili ya kushambulia".
"Kitu pekee kizuri ilikuwa ni kumrudisha Mosimane na wachezaji wake katika akili zao baada ya kulewa mafanikio ya kushika nafasi ya tatu katika michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia," alisema.
Wakati Ahly itaikaribisha Vita, ambayo haitabiriki, Simba itakuwa ugenini kumenyana na Al Merreikh, klabu ya Sudan ambayo imepata vipigo viwili mfululizo va tofauti ya mabao matatu.

Wydad yategemea ushindi
Katika Kundi B, Wydad imekuwa moja ya timu zinazofanya vizuri Ligi ya Mabingwa katika misimu ya karibuni, ikiwa imetwaa ubingwa, kushika nafasi ya pili na kufika nusu fainali mara mbili katika misimu mitano iliyopita.
Ikifundishwa na kocha vedterani, Faouzi Benzarti, inajivunia wachezaji nyota kama mshambuliaji Ayoub el Kaabi na kiungo Mlibya, Muaid Ellafi.
Wydad itakuwa inategemewa kushinda nyumbani dhidi ya Horoya ya Guinea, wakati Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini na Petro Atletico ya Angola zinapambana jijini Soweto, zikisaka pointi zote ili ziendelee kubaki katika kuwania tiketi ya kusonga mbele.
Katika Kundi C, kocha wa Sundowns, Manqoba Mngqithi ameonya dhidi ya kujiamini kupita kiasi wakati timu hiyo ikijiandaa kuivaa TP Mazembe, ambayo imeshatwaa ubingw wa Afrika mara tano, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Themba Zwane alifunga mabao mawili wakati klabu hiyo ya Pretoria ilipoisambaratisha CR Belouizdad kwa mabao 5-1 mwishoni mwa wiki iliyopita, lakini Waalgeria hao walicheza dakika 87 pungufu baada ya Chouaib Keddad kuonyeshwa kadi nyekundu.
"Tulisaidiwa na kadi nyekundu iliyotolewa mapema, lakini bado hatukuonyesha uwezo wetu wa kutawala mchezo hadi kipindi cha pili. Mchezo wetu wa dakika za mwanzo hautakiwi ujirudie dhidi ya Mazembe."
Ratiba ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) haikuwa kubwa zaidi ya Esperance ya Tunisia dhidi ya Zamalek ya Misri, ambao kwa jumla wametwaa ubingwa wa Afrika mara tisa.
Esperance itakuwa nyumbani na inaongoza kwa tofauti ya pointi mbili dhidi ya Zamalek, ambayo haijaweza kufunga bao ilipotoka sare na Mouloudia Alger ya Algeria na Teungueth ya Senegal inayoshiriki kwa mara ya kwanza.
Ingawa Watunisia hao walitikisa mabao sita katika mechi nne za michuano ya awali na hakuna mchezaji ambaye amefunga zaidi ya bao moja, kitu ambacho kocha Moine Chaabani inabidi akiangalie. 
Mechi za Jumamosi
Al Merrikh (SUD)    v Simba (TAN)
Al Ahly (Misri)        v VIta Club (DRC)
Msimamo:
Simba      2 2 0 0 2 0 6
V Club     2 1 0 1 4 2 3
Ahly       2 1 0 1 3 1 3
Merrikh    2 0 0 2 1 7 0

Kundi B
Leo
CR Belouizdad (ALG)    v Al Hilal (SUD)
Jumamosi
TP Mazembe (DRC)    v Mamelodi Sundowns (RSA)
Msimamo:
Sundowns   2 2 0 0 7 1 6
Mazembe    2 0 2 0 0 0 2
Hilal      2 0 1 1 0 2 1
Belouizdad 2 0 1 1 1 5 1

Kundi C
Jumamosi
Kaizer Chiefs (RSA)    v Petro Luanda (ANG)
Wydad Casablanca (MOR)    v Horoya (GUI)
Msimamo
Wydad      2 2 0 0 5 0 6
Horoya     2 1 1 0 2 0 4
Chiefs     2 0 1 1 0 4 1
Petro      2 0 0 2 0 3 0

Kundi D
Jumamosi
Esperance (TUN)        v Zamalek (MIS)
Teungueth (SEN)        v Mouloudia Alger (ALG)
Msimamo:
Esperance  2 1 1 0 3 2 4
Mouloudia  2 0 2 0 1 1 2
Zamalek    2 0 2 0 0 0 2
Teungueth  2 0 1 1 1 2 1

*Washindi wawili wa kila kundi wanafuzu kucheza robo fainali.