Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo mawili kwa Yanga vs Namungo leo

Muktasari:

  • Mechi hii inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka kutokana na ubora wa timu hizo, lakini pia rekodi zao kwenye michezo kadhaa iliyopita.

Dar es Salaam. Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga, leo wanaingia uwanjani kucheza mechi muhimu dhidi ya Namungo ya Lindi, kwenye mchezo utakaopigwa Uwanja wa Majaliwa, ikiwa na mambo mawili muhimu.

Mechi hii inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka kutokana na ubora wa timu hizo, lakini pia rekodi zao kwenye michezo kadhaa iliyopita.

Yanga itashuka kwenye mchezo huu ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo baada ya kushushwa na Azam FC, ilipotoka sare ya bao 1-1 na Dodoma Jiji juzi na kufikisha pointi 44, ikiwa ni moja mbele ya Wanajangwani hao.

Hivyo jambo la kwanza, Yanga itashuka kwenye mchezo huo, ikitambua kwamba inatakiwa kushinda ili kuwa na gepu kubwa kati yake na watani wao wa jadi Simba ambao juzi walipoteza mchezo wa pili kwenye ligi baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Prisons na kubaki nafasi ya tatu na pointi 36, saba nyuma ya Yanga.

Lakini jambo la pili, Yanga itatakiwa kupambana ili kuhakikisha inapata ushindi na kurejea kileleni mwa msimamo sehamu ambayo imekaa muda mrefu kuanzia msimu huu wa ligi kuu umeanza.

Yanga imekuwa ikikutana na wakati mgumu kila inapocheza na Namungo, katika mechi tisa zilizopita, Yanga imeshinda tano, huku nne timu hizo zikitoka sare hivyo takwimu hizo zinaonyesha kuwa mechi ya leo haiwezi kuwa rahisi.

Hata hivyo, Yanga imekuwa na wakati mgumu kushinda dhidi ya Namungo ugenini, kwani kwenye michezo minne imepata ushindi mara moja na mara tatu timu hizo zikienda sare.

Kwenye michezo hiyo, Namungo ambayo ipo chini ya kocha wa zamani wa Yanga Mkongomani, Mwinyi Zahera, imefungwa mabao 13 nayo ikifunga sita pekee, hivyo ni lazima leo ipambane kulinda zaidi lango lake.

Kwenye mechi tano zilizopita, Namungo imepata ushindi mara moja tu ikitoa sare michezo mitatu na kupoteza mechi moja, huku Yanga ikiwa na matokeo bora ikitoa sare mchezo mmoja na ikishinda mechi nne mfululizo zilizopita.

Akizungumzia mchezo huo jana, Meneja wa Habari wa Yanga, Ally Kamwe, alisema hawatarajii mechi nyepesi kutokana na ubora wa Namungo kwenye ligi kwa sasa, lakini upinzani ambao wamekuwa wakiuonyesha kila wanapokutana.

"Tuna michezo minne mbele yetu inatusubiri ambayo ina jumla ya pointi 12, ambazo tunazitaka, tunaanza na mechi dhidi ya Namungo halafu tutacheza na Ihefu, Geita Gold na Azam FC, safari inaanzia hapa na tunakwenda kwenye mechi hii tukiwa na umoja, mshikamano na ari, tukiwa tunafahamu kuwa tunakutana na timu bora kwenye ligi kwa sasa," alisema Kamwe.


Dondoo za Ligi Kuu Bara
Wafungaji;

Feisal Salum:    12
Stephen Aziz Ki: 10
Jean Baleke:     8
Maxi Nzengeli:   8


Vinara wa kufunga mabao ya penalti;
Saido Ntibazonkiza: 4
Fabrice Ngoy:      1
Daniel Lyanga:     1
Prince Dube:       1.


Mabeki wenye pasi nyingi za mabao;

Kouassi Yao      :6
Pascal Msindo    :4
Nickson Kibabage :4
Lusajo Mwaikenda :4