Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ruud van atua Man United

Muktasari:

  • United leo imejikusanya kwa ajili ya kuanza safari ya kwenda Norway kuvaana na Rosenborg Jumatatu  ijayo ukiwa ni mchezo wake wa kwanza wa    maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu England na michuano mingine.

Manchester, England. Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Ruud van Nistelrooy leo ametua kwenye kikosi hicho kuanza kazi chini  Erik ten Hag.

United leo imejikusanya kwa ajili ya kuanza safari ya kwenda Norway kuvaana na Rosenborg Jumatatu  ijayo ukiwa ni mchezo wake wa kwanza wa    maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu England na michuano mingine.

Baada ya kuongeza mkataba wa kuifundisha United hadi mwaka 2026 , Ten Hag ameachana na wasaidizi wake kadhaa na kumchukua Van Nistelrooy, ambaye alifunga mabao 150 kwa kipindi cha miaka mitano aliyokaa Old Trafford.

Gari la Ruud van Nistelrooy ambaye bado hajatangazwa rasmi na United lilikuwa la tano kuingia kwenye uwanja wa mazoezi ikiwa ni mara yake ya kwanza kuwa kocha wa timu hiyo baada ya kuondoka hapo akiwa mchezaji mwaka 2006 akiwa ametumika kwenye misimu mitano.

Van Nistelrooy ataungana na wageni wengine Rene Hake ambaye ameachana na Go Ahead Eagles ambapo alikuwa kocha mkuu na kukubali kuwa msaidizi wa Ten Hag ambaye msimu uliopita aliipa United ubingwa wa Kombe la FA.

Awali klabu ya Burnley ilikuwa inamtaka Van Nistelrooy, baada ya kuachana na Vincent Kompany lakini taarifa zinasema kuwa aligomea kibarua hicho na kukubali kutua United.

Mbali na kuwa mchezaji mahiri, Ruud Van mwenye miaka 48 amefanya kazi nzuri akiwa kocha wa Akademi ya PSV Eindhoven, lakini pia amefanya kazi kama msaidizi wa kocha mkongwe Guus Hiddink kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi.

Machi 2022 alitangazwa kuwa kocha mkuu wa  PSV ya nchini kwao.

Pamoja na kwamba alifanya vizuri kwa kutwaa ubingwa wa Johan Cruyff Shield na KNVB Cup, Van Nistelrooy alijiuzulu kwa sababu ya kukosa ushirikiano wa kutosha klabuni hapo.

Kwa upande wa Hake, huyu siyo mgeni kwa  Ten Hag wakiwa wamefanya kazi pamoja FC Twente  na timu ya mwisho ilikuwa Eagles ambapo walimaliza msimu wa Ligi Kuu Uholanzi wakiwa nafasi ya tisa.

“Nina furaha kuona naungana tena na Te Hag ni mtu ambaye tumefanya kazi pamoja kwa mafanikio makubwa, ni ngumu kueleza jinsi ambavyo tumekuwa tukishirikiana, lakini naamini pia hapa tutafanya kazi nzuri,”alisema Hake.

Mbali na hao, United pia imemchukua kocha wa makipa  Jelle ten Rouwelaar, kutoka Ajax ambaye atakuwa kwenye kikosi hicho msimu ujao.

Benni McCarthy ambaye alikuwa kocha wa washambuliaji anatarajiwa kuondoka kwenye kikosi hicho kutokana na mkataba wake kumalizika, pia timu hiyo ipo kwenye mazungumzo ya kuachana na Stephen McClaren ambaye amekuwa kwenye kikosi hicho kwa muda mrefu.