Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Prof Mukandala kuheshimisha UDSM kwa kutoa Mhadhara wa Uprofesa

Profesa wa Sayansi ya Siasa na Utawala, Profesa wa Kigoda cha Mwalimu J. K. Nyerere katika Taaluma za Umajumui wa Afrika, na Makamu Mkuu wa Chuo Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rwekaza Sympho Mukandala.

Dar es Salaam. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ni kiwanda kilichozalisha wasomi wengi ikiwamo maprofesa na madaktari wa kada za uchumi, sayansi, uhandisi, siasa na nyinginezo ambao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakipishana katika nafasi za kimaamuzi za Taifa hili.

Profesa Rwekaza Mukandala ambaye amewahi kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni miongoni mwa majina yanayokuja haraka kichwani unapofikiria wasomi waliojijengea heshima kubwa hapa nchini kwa kusaidia utatuzi wa masuala mbalimbali ya kijamii.

Tangu atunukiwe Shahada yake ya Uzamivu katika Sayansi ya Siasa na Uongozi wa Umma mwaka 1988 katika Chuo Kikuu cha Berkeley, California, Marekani na kurejea nchini akiwa kama mhadhiri mwandamizi chuoni hapo, hadhi ya UDSM iliendelea kupanda siku baada ya siku.

Ukumbi wa Mikutano wa Nkrumah uliopo ndani ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) utakaotumika kuendeshea Mhadhara wa Uprofesa Mei 21, 2024.

Mwaka 2016, Profesa Mukandala alikasimiwa nafasi ya Makamu Mkuu wa Chuo na chuo hicho kiliendelea kusimama kama moja ya alama kuu ya elimu ya juu nchini.

Kabla ya hapo, aliwahi kuwa mlezi wa Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Jamii, Mkuu wa Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala wa Umma.

Licha ya kuvutia wanafunzi wapya chuoni hapo, lakini idadi ya miradi ya utafiti iliongezeka maradufu, vitivo na kozi mpya zilianzishwa chini ya uongozi wake.

Mbali na nafasi alizoshika ndani ya chuo, ikumbukwe kuwa Profesa Mukandala amekuwa akihudumu katika nyadhifa mbalimbali katika taasisi kama vile; Mpango wa Utafiti wa Elimu ya Demokrasia nchini (REDET), Taasisi ya Uangalizi wa Uchaguzi Tanzania (TEMCO), Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Taasisi ya Uongozi ya Afrika Mashariki (EAFUI), Chama cha Sayansi ya Siasa barani Afrika (AAPS) na Chama cha Kimataifa cha Sayansi ya Siasa (IPSAS).

Pia, amehudumu katika Baraza la Utawala la Taasisi ya Kimataifa ya Sayansi za Utawala. Katika muongo mmoja uliopita, amejipambanua katika tafiti za sayansi ya siasa, misaada, wahisani katika nchi nyingi za Kiafrika. Kama hiyo haitoshi, Afrika inamtambua kama miongoni mwa wanamajumui wakubwa kupitia uchapishaji wa vitabu zaidi ya 15 na makala zaidi ya 60 katika majarida ya ndani na kimataifa.

Kwa wale waliopita katika mikono yake kitaaluma, watakuambia kuwa Profesa huyo alikuwa pia mahiri wa kutumia lugha adhimu ya Kiswahili katika hadhara zake.

Licha ya maarifa makubwa yaliyopo kichwani mwake, lakini ni mtu mwenye haiba ya Kizalendo, akiamini kuna daraja linalotenganisha maarifa na lugha.

Na huu ndiyo upekee wa Profesa Mukandala na wasomi wengine waliopo nchini. Yapo mengi ya kumwelezea Profesa ili kizazi cha leo na kijacho kimwelewe kwa undani lakini inaweza kuhitaji pengine nusu ya gazeti hili kukamilisha wasifu wake.

Mhadhara wa Uprofesa Baada ya kumaliza utumishi wake katika nafasi ya Makamu Mkuu wa Chuo cha UDSM, imekuwa ngumu kumsoma magazetini na mitandaoni au kumsikia Profesa Mukandala katika vichwa vya habari.

Lakini, hata kundi la wale waliohitimu chuoni hapo bado wanashauku ya kumsikia Profesa akihadhiri ili kupata maarifa mapya wakati nchi yetu ikiendelea kupitia vipindi mbalimbali.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Utafiti, Profesa Nelson Boniface anasema kwa kuthamini mchango wake katika taaluma nchini, uongozi wa UDSM unatarajia kuandaa mhadhara wa Uprofesa Mei 21, 2024 utakaofanyika katika ukumbi wa Nkrumah, kuanzia majira ya saa 8:00 mchana.

Mhadhara huo, kulingana na Profesa Boniface, utatolea ufafanuzi mada mbalimbali ikiwamo; Dola, Soko, Kushindwa kwa Taasisi, Mafunzo kutoka katika Kujifungua kwa Uchungu wa Kushinikiza, Maisha ya Mateso, na Kifo cha Maumivu Cha MV. Bukoba.

Akiwa mwanazuoni, mtafiti, mwalimu, na kiongozi mahiri aliyebobea katika nyanja za Utawala wa Umma, Siasa Linganishi na Utawala wa Kidemokrasia, anasema atatumia mbinu anuai za kihistoria zenye mseto wa taaluma kuanzia fizikia hadi sayansi ya siasa, sheria na uchumi, kuchunguza kiini cha kile kinachohitimishwa kuwa ni kujifungua kwa uchungu wa kushinikiza, maisha ya mateso, na kifo cha maumivu cha MV. Bukoba.

Hatimaye, tukio hili litatumika kutoa mafunzo muhimu kwa sasa na baadae.

Katika mhadhara huu, Profesa Mukandala pia anakusudia kuonyesha mchango wa Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika kusaidia kupatikana kwa maendeleo endelevu ya Tanzania kwa kuainisha mbinu madhubuti katika menejimenti ya majanga na maafa, utawala wa umma na utawala bora.