Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CCM Dar ilivyoteua, engua wagombea udiwani

Muktasari:

  • Hadi kukamilika kwa mchakato wa uteuzi huo umefanyika kwa ngazi tatu ambazo ni kukagua wagombea waliokidhi masharti ya msingi, kuchagua wagombea kwa ngazi ya Wilaya na kukamilisha uteuzi wa wagombea kwa kupitia sekretarieti ya Taifa ya chama.

Dar es Salaam. Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam imekamilisha uteuzi wa wagombea udiwani na udiwani wa viti maalumu watakaowakilisha chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Kikao hicho kilifanyika jana Jumatano, Agosti 13, 2025, katika ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 14, 2025, Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ally Bananga amesema kikao cha halmashauri kuu kiliazimia na kuteua kwa asilimia 99.02 wagombea waliokuwa na nafasi ya juu kwenye kura za maoni katika kata zote 102.

“Tumefanya mkutano maalumu wa kata, wilaya na Taifa kuhakikisha wagombea wote wanakidhi vigezo na wanachaguliwa kwa haki bila rushwa au hila yoyote,” amesema Bananga.

Bananga amesema uteuzi huo umezingatia kwa karibu kanuni za uteuzi wa wagombea uongozi katika vyombo vya Dola, hasa Kanuni ya 9(1) inayoeleza kuwa:

“Mgombea yeyote wa CCM anayetaka kuingia katika chombo cha dola, atateuliwa kwa kuzingatia kura za maoni zilizopigwa. Mgombea atakayeteuliwa ni yule anayeongoza kwa wingi wa kura za maoni alizopata.

Isipokuwa kwamba endapo itathibitika kura hizo za ushindi amezipata kwa njia ya rushwa, kikao cha uteuzi wa mwisho hakitamteua."

Amesema hadi kukamilika kwa mchakato wa uteuzi huo, umefanyika kwa ngazi tatu ambazo ni kukagua wagombea waliokidhi masharti ya msingi, kuchagua wagombea kwa ngazi ya wilaya na kukamilisha uteuzi wa wagombea kupitia sekretarieti ya Taifa ya chama.

Bananga amesema katika kata 102 ni kata moja ambayo uteuzi wake haujafanyiwa kazi kutokana na changamoto za kisheria ambayo ni Kata ya Buyuni katika jimbo la Kivule.

Mbali na kata hiyo, kwa upande wa jimbo la Kigamboni kata ya Vijibweni limerudishwa jina la Zacharia Mkundi ambaye aliongoza kwa kura badala ya Nicolaus Mlanda ambaye jina lake lilipelekwa mkoani kimakosa.

"Tulishatoa maelekezo ya watu watakaoongoza kwa kura kupewa nafasi katika kata ya vijibweni, limekuja jina la mtu mwingine kimakosa na sasa linafanyiwa kazi kuweka mambo sawa, "amesema Bananga.

Katika waliorudishwa baada ya wajumbe kuandamana akiwemo aliyekuwa diwani wa Kunduchi Michael Urio ambaye kwenye kura za maoni aliongoza, lakini nafasi yake imechukuliwa na aliyeshika nafasi ya pili Joyce Haule.


Urejeshaji wa majina

Bananga amesema uamuzi wa kurejesha baadhi ya majina ya wagombea ambao awali yaliondolewa katika mchujo ni hatua ya kuongeza wigo wa demokrasia ndani ya chama, baada ya kubaini ushindani mkubwa na wagombea wengi wenye sifa zinazokaribiana.

Amesema awali mchakato wa kura za maoni ulipitia hatua kadhaa, ikiwemo kuwapa nafasi waliokuwa madarakani, kuhakikisha usawa wa kijinsia na kisha kuzingatia ushindani katika maeneo yenye wagombea wengi.

“Kwa mfano, pale kulipokuwapo na mgombea mwanamke na diwani aliyekuwa madarakani, ilibidi tupunguze idadi kwa kipaumbele cha usawa wa kijinsia. Lakini tulipoona nafasi inabaki moja na bado wagombea wengi walikuwa na sifa, tuliona tumezuia kidemokrasia kwa kiwango fulani,” amesema Bananga.

Ameeleza baadhi ya waliorejeshwa walionekana kufanya vizuri katika hatua ya pili ya mchujo, licha ya kuondolewa awali, na kwamba hatua hiyo imewapa nafasi bora zaidi chama kupata wagombea waliopimwa kwa kina.

“Ni kama tunavyochuja pombe ya gongo. Hawa wamepitia chujio la kwanza, wakapita tena la pili. Wamechujwa, wakachaguliwa, na kuteuliwa. Sasa chama chetu hakina biashara ya upendeleo, lazima upitie mchakato,” amefafanua.

Bananga amesema demokrasia ya kweli inahitaji taratibu kubwa na wakati mwingine maumivu, hasa kwa wale waliokuwa wakitarajia kushinda lakini wakaanguka, ikiwemo madiwani wa zamani na manaibu meya.

Amesifu uongozi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam unaoongozwa na Abassi Mtengu na Elia Simpanda kwa kuhakikisha mchakato umetulia bila malalamiko makubwa.

“Kila mmoja ameridhika, tumewaangusha majina makubwa, tumewaacha wengine, lakini wote wamekubali matokeo. Hii ndiyo roho ya demokrasia,” amesema.

Bananga amesisitiza maandalizi haya ni sehemu ya kujipanga kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025, na chama kimeonesha mfano wa kuigwa katika kuendesha mchakato wake kwa uwazi na uadilifu.

Mchanganuo wa Uteuzi

Bananga amesema wilaya tano, kata 102 ndani ya mkoa wa Dar es Salaam wilaya ya Ilala ina majimbo manne kata 36.

Majimbo hayo ni Ilala kata 10 ambapo wagombea wa zamani walirudishwa ni saba na wapya watatu. Jimbo la Kivule likiwa na kaya sita huku wagombea wa zamani ni watatu na wapya watatu.

Jimbo la Ukonga kata saba wagombea wa zamani mmoja wapya sita huku Jimbo la Segerea ikiwa na kata 13 ambapo wagombea wa zamani ni saba na wapya sita.

Kwa upande wa Wilaya ya Temeke ikiwa na majimbo manne ambapo jimbo la Temeke linakata 13 wagombea wa zamani 11 na wapya sita.

Jimbo la Mbagala lina kata sita wagombea wa zamani hakuna na wapya ni sita na Jimbo la Chamazi lina kata nne ambapo wagombea wa zamani ni mmoja na wapya watatu.

Katika Jimbo la Kigamboni lenye kata tisa, wagombea wa zamani ni sita huku wapya wakiwa watatu.

Katika wilaya ya Ubungo Bananga amesema ina kata 14 ambapo Jimbo la Ubungo lenye kata nane wagombea wa zamani wanne na wapya wanne.

Katika Jimbo la Kibamba amesema lina kata sita ambapo wagombea wa zamani hakuna huku wapya wakiteuliwa sita.

Katika Wilaya ya Kinondoni amesema lina majimbo mawili la Kinondoni lenye kata 10 na walioteuliwa wa zamani watano, wapya watano na kwa upande wa Kawe kata 10 ambapo wa zamani wawili na wapya wanane.