Dk Bashiru atua Zanzibar kuiimarisha CCM

Tuesday November 26 2019

 Bashiru -atua- Zanzibar -kuiimarisha -CCM-Katibu- Mkuu - chama- tawala -nchini -Tanzania-ziara-unguja-pemba-visiwani-chama-mwananchiHabari-MwananchiGazeti-

 

By Muhammed Khamis, Mwananchi [email protected]

Unguja. Katibu Mkuu wa chama tawala nchini Tanzania cha CCM, Dk Bashiru Ally amewasili visiwani Zanzibar kwa ziara ya siku 10 Unguja na Pemba visiwani Zanzibar.

Dk Bashiru aliwasili jana usiku Jumatatu Novemba 25, 2019 visiwani humo na kusema, “nimekuja kwa ziara ya kukijenga chama, wembe ni ule ule.”

Alisema kwa upande wa Tanzania bara tayari jitihada kubwa zimefanyika kukikuza chama chake na kwamba sasa ni wakati wa Zanzibar.

Alisema katika ziara yake itakayohitimishwa Desemba 4, 2019 itajikita zaidi na ujenzi wa chama katika kila eneo ambapo Unguja atatumia siku tano na Pemba siku nne, “itakuwa asubuhi hadi asubuhi siku inayofuata.”

“Kwa sababu ya kazi inayofanywa na chama hichi ndio maana tumeshinda maeneo yote ya serikali za mitaa kwa upande wa Tanzania bara hivyo ni lazima matokeo haya yaendelezwe,” alisema

 

Advertisement

Endelea kufuatilia Mwananchi kujua kinachojiri kwenye ziara hiyo

Advertisement