Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pedeshee Didi Kinuani azushiwa kifo

Mfanyabiashara maarufu na mdau mkubwa wa muziki wa dansi nchini DR Congo, Didi Dedace Kinuani 'Dikin' a.k.a Didi Stone.

Muktasari:

  • Didi anayejishughulisha na biashara mbalimbali ikiwamo kuuza madini ya Almasi aliandika ujumbe na kueleza yu salama, huyu bintie naye Leatitie Muadi akieleza taarifa za kifo chake ni habari za uzushi.

Kinshasa. Mfanyabiashara maarufu na mdau mkubwa wa muziki wa dansi nchini DR Congo, Didi Dedace Kinuani 'Dikin' a.k.a Didi Stone, amezushiwa kifo huku mwenyewe akiibuka na kukanusha taarifa hizo akisema yu mzima buheri wa afya.

Taarifa za Didi Kimuani kudaiwa kufariki dunia zilianza kusambaa mapema leo Jumatatu, Machi 4, 2024 kwenye mitandao ya kijamii.

Pedeshee huyo, ambaye ni mmiliki na mkurugenzi wa kampuni za Dikin Investment, ilidaiwa amekumbwa na mauti jana akiwa nchini humo, huku taarifa zingine zikisema alifariki dunia akiwa Luanda, Angola.

Hata hivyo, chanzo cha kifo chake akijabainishwa waziwazi, ila inaelezwa aliumwa ghafla na aliaga dunia akiwa anapatiwa matibabu.

Hata hivyo, kupitia akaunti yake ya X, bilionea huyo aliyeimbwa kwenye nyimbo kadhaa za wanamuziki wa Kicongo akiwamo swahiba wake mkubwa, Koffi Olomide, Werrason Ngiama Makanda, Red Amisi, kundi la Victoria Ellyson na wengineo alikanusha uzushi huo akisema yu hai.

Didi anayejishughulisha na biashara mbalimbali ikiwamo kuuza madini ya Almasi aliandika ujumbe huo kueleza yu salama, huyu bintie naye Leatitie Muadi akieleza taarifa za kifo chake ni habari za uzushi.

Koffi Olomide akiwa na binti yake, Didi Stone. Koffi alimpa jina hili kwa ajili ya kudumisha ushwahiba wake na bilionea, Didi Kinuani ambaye pia ni maarufu kama Didi Stone.

Bilionea huyo aliwahi kutajwa kama ni mmoja wa washirika wakubwa wa Joseph Kabila aliyekuwa Rais wa DR Congo na amekuwa akisifika kwa kujitolea kuwasaidia wanamuziki na madansa wa taifa hilo wakiwemo wananchi wa eneo alilozaliwa la Bandundu.

Inaelezwa pia amekuwa akitumia utajiri wake wa kuuza madini kujenga hospitali na huduma nyingine za kijamii huko DR Congo na Angola alipokuwa na maskani yake.

Didi anakumbukwa zaidi kwa tukio la kumpora mke, kiongozi wa zamani wa Wenge Musica BCBG, JB Mpiana mwanzoni mwa miaka ya 2000.

JB Mpiana alifunga ndoa na mrembo maarufu Amida Shatur, shombe shombe wa Kilebanon na kuzaa naye watoto watatu. Hata hivyo, baadaye walitengana huku chanzo kikielezwa kuwa ni Didi na taarifa zingine zikimtaja Spika wa Bunge wa zamani wa DR Congo, Vital Kamerhe.

Hata hivyo, mambo yalikuwa hadharani baada Didi na Amida kufunga ndoa mwaka 2003 na wawili hao kujaaliwa kupata mtoto mmoja, Diam ikiwa ni kifupi cha majina ya Didi na Amida.

Licha ya kuwa Amida na JB walikuja kurudiana baadaye, lakini waliachana tena baada ya mrembo huyo kudaiwa kuanzisha uhusuano na Vital.

Umaarufu wa Amida nchini DR Congo umekuwa kwa kasi kutokana na kuimbwa kwenye nyimbo kadhaa za JB kabla na baada ya Wenge Musica 4x4 kusambaratika mwaka 1998.

Uswahiba wa Didi na Koffi umetajwa kuota mizizi kwa muda mrefu gwiji huyo wa muziki barani Afrika kumpa jina la Didi Stone mmoja ya watoto wake wa kike. Koffi amekuwa akilitaja sana jina la Didi Stone kwenye nyimbo zake.

Mbali na Didi Kinuani, wafanyabiashara wengine maarufu wanaotamba kwa kuimbwa kwenye nyimbo za wanamuziki wakubwa nchini DR Congo ni mwanamama mwenye fedha zake, Jose Kongolo anayeishi nchini Ufaransa, Mohammed Kanyasi na Etienne Mundele.