Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Soksi ya Michael Jackson yauzwa Sh20 milioni

Muktasari:

  • Dalali wa soksi hiyo tokea Ufaransa amesema Michael Jackson alivaa soksi nyeupe zilizopambwa kwa vifaru vinavyometameta wakati wa tamasha la muziki la 'History World Tour' mnamo 1997.

Marekani. Soksi moja ya mfalme wa muziki wa Pop duniani, Michael Jackson ambayo aliivaa wakati wa tamasha nchini Ufaransa mwaka 1997, imeuzwa kwa zaidi ya dola 8,000 zaidi ya Sh20 milioni.

Dalali wa soksi hiyo tokea Ufaransa amesema Michael Jackson alivaa soksi nyeupe zilizopambwa kwa vifaru vinavyometameta wakati wa tamasha la muziki la 'History World Tour' mnamo 1997.

Inaelezwa kuwa soksi hiyo iliokotwa na fundi mmoja ikiwa imetupwa karibu na chumba alichobadilishia nguo Michael Jackson baada ya tamasha hilo katika mji wa Nimes Julai 1997, dalali Aurore Illy aliiambia AFP.

Hata hivyo, Michael Jackson alionekana akiwa amevalia soksi hiyo kwenye baadhi ya vipande vya video, wakati akitumbuiza wimbo wake wa "Billie Jean".

Miongo kadhaa baadaye, soksi hiyo imeuzwa tena kwa pesa ndefu huku dalali Aurore Illy akisema soksi hiyo inaweza kutumika kama ibada kwa mashabiki wa Michael Jackson.

"Kwa kweli ni kitu cha kipekee soksi hiyo inaweza kuwa hata ibada kwa mashabiki wa Michael Jackson," alisema Illy.

Utakumbuka hii sio mara ya kwanza kwa vitu vya Michael Jackson kupigwa mnada mwaka 2009 kituo cha michezo cha Macau kililipia  dola 350,000 ili kununua glavu ya kumeta meta ambayo MJ alivaa wakati akitumbuiza ngoma yake ya kwanza ya 'moonwalk' mwaka 1983. Pia kofia aliyovaa kabla tu ya maonyesho hayo iliuzwa kwa zaidi ya dola 80,000 huko Paris mwaka 2023.

Michael Jackson alifariki dunia mwaka 2009 akiwa na miaka 50. licha ya kifo chake na tuhuma za unyanyasaji wa watoto wakati wa uhai wake na baada ya kifo bado mfalme huyo wa Pop duniani anawafuasi wengi ambao mpaka leo wanaendelea kuonesha mapenzi yao kwake.