Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makamu wa Rais awaonya wanaobambika wananchi bili za maji

Muktasari:

Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango amevitaka vyombo vya usalama nchini kuwafuatilia na kuwachukulia hatua kali za kisheria watu na wawekezaji wakubwa wanaoiba maji na wanaochepua maji kutoka kwenye mito bila vibali wabomoe vizuizi walivyojenga na waache mara moja tabia hiyo.

Shinyanga. Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango amevitaka vyombo vya usalama nchini kuwafuatilia na kuwachukulia hatua kali za kisheria watu na wawekezaji wakubwa wanaoiba maji na wanaochepua maji kutoka kwenye mito bila vibali wabomoe vizuizi walivyojenga na waache mara moja tabia hiyo.

Pia, amewataka watumishi wa Shuwasa wanaosoma bili za maji waache kuwabambikia bili wateja wao kwani baadhi ya wananchi wamekuwa wakilalamika kuwa wasoma mita wamekuwa hawafiki kusoma mita hivyo kuwabambikizia hivyo wanatakiwa waache tabia hiyo watoe bili zinazotakiwa.

Maagizo hayo ameyasema leo wakati akiweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji ya Ziwa Victoria katika kijiji cha Buchama kata ya Tinde halmashauri ya Shinyanga, ambapo amesema maagizo hayo aliyoyatoa yafanyiwe kazi kwa wakati ili kuondoa malalamiko hayo.

"Nasisitiza haya yatekelezwe kwa haraka ili wananchi waweze kutendewa haki na naomba mradi huu utekelezwe kwa haraka ili wananchi waweze kunufaika na mradi huu. Pia namuomba Waziri wa Maji na watu wako msimamie suala la wizi wa maji, ili kuondoa malalamiko kwa wananchi," amesema Makamu wa Rais Mpango.

Mbunge wa Jimbo la Solwa, Ahamed Salumu amemshukuru Makamu wa Rais Dk Mpango kwa kuweka jiwe la msingi katika mradi wa Ziwa Victoria kwenda mji wa Tinde ambao utahudumia wananchi zaidi ya 6,000 katika vijiji 22 vya Halmashauri ya Shinyanga. Pia ameomba Sh6 bilioni kwa ajili ya kuleta maji katika vijiji 20 vilivyobaki.

Amesema Jimbo la Shinyanga lina vijiji 126 vijiji 59 tayari vimeshaanza kutumia maji safi na salama kabla ya mradi huo. Hivyo amemuomba Makamu wa Rais fedha za kuweza kujenga vituo vya afya vitatu katika Wilaya ya Shinyanga ambavyo vitajengwa katika Kata za Lyabukande, Didia na Mwakitolyo.


"Mheshimiwa Makamu wa Rais kuna barabara za lami zipo kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi, barabara ya kutoka Solwa kwenda Mwanza. Pia amemuombea Mbunge wa Kishapu barabara ya kutoka Shinyanga kwenda Kishapu apatiwe fedha kwa ajili ya kutengeneza barabara yenye kiwango cha lami," amesema Mbunge Salum.