Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Berege: Jiungeni TUCTA kurahisisha utatuzi migogoro

Muktasari:

Serikali imeshauri njia ya kuungana kwa vyama vyote vya wafanyakazi ili kuweka urahisi wa kutatua changamoto na migogoro mahala pa kazi.

Morogoro. Msajili wa vyama vya wafanyakazi nchini, Pendo Berege amevishauri vyama hivo ambavyo bado havijajiunga na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) kujiunga ili kuleta ufanisi kwenye masuala ya wafanyakazi na utatuzi wa migogoro.

Amesema hayo leo Jumatano Mei 17, 2023 mkoani Morogoro katika kikao cha watendaji, waajiri na mashirikisho ya vyama hivyo ambapo ameeleza lengo la kikao hicho ni kukumbushana wajibu na majukumu katika utekelezaji wa katiba na kanuni za vyama.

Berege amesema katika vyama 33 vilivyosajiliwa nchini ni vyama 13 tu vimejiunga TUCTA huku vyama 5 vikiwa vimeingia kwenye mchakato wa kujiunga na shirikisho hilo.

“Vyama vyote vikijiunga na TUCTA tutakuwa na uwezo wa kukaa kwa pamoja na kwa umoja wao kama watendaji wa vyama kujadiliana kuhusu haki za wafanyakazi kwenye maeneo ya kazi,’’ amesema.

Naye, Rais wa TUCTA, Tumaini Nyamhokya amewataka viongozi wa vyama hivyo kuwafikia wanachama wao kwa wakati ili kuepusha migogoro isiyokuwa na lazima mahala pa kazi.

Amesema ili vyama vifanikiwe vinapaswa kuwa na nguvu ya kiuchumi ili wanachama wafikiwe kwa wakati wanapohitaji msaada.

"Pamoja na migogoro kupungua maeneo pa kazi lakini bado ni changamoto kubwa na hii inatokana na vyma kutokuwa pamoja, kuna ambavyo havijajiunga na TUCTA, hii sio afya kwa wanachama wetu. Niwaombe wenzetu mlioko nje mjiunge tuwe pamoja,"amesema Nyamhokya.

Mwakilishi kutoka Chama cha Waajiri Tanzania (Ate), Leonard Selestine amesema suala la afya mahala pa kazi ni muhimu kuzingatiwa kwa wafanyakazi kwa kuwa linaongeza tija na uzalishaji kazini.

Aidha, ameshauri wafanyakazi kuepuka vitendo na vishawishi vinavyosababisha rushwa mahali pa kazi na badala yake kutekeleza majukumu ya kazi kama inavyotakiwa.