Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chanjo yaanza kusambazwa mikoa 26

Muktasari:

  • Baada ya taasisi tano zilizo chini ya wizara ya afya na maabara kuu ya taifa kufanya uchunguzi na kujiridhisha kuwa chanjo za Johnson&Johnson ni salama kutumika kwa Watanzania, zimeanza kusafirishwa mchana huu katika mikoa 26 kwa ajili ya makundi matatu yaliyopewa kipaumbele wakiwemo watoa huduma za afya, wazee na wenye magonjwa sugu.

Dar es Salaam. Baada ya taasisi tano zilizo chini ya wizara ya afya kufanya uchunguzi na kujiridhisha kuwa chanjo za Johnson & Johnson ni salama kutumika kwa Watanzania, zimeanza kusafirishwa mchana huu katika mikoa 26 kwa ajili ya makundi matatu yaliyopewa kipaumbele wakiwemo watoa huduma za afya, wazee na wenye magonjwa sugu.

Taasisi zilizochunguza chanjo hiyo ni pamoja na Mkemia Mkuu wa Serikali, Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu NIMR, Chuo Kikuu cha Sokoine SUA, Muhimbili na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA).

Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Profesa Abel Makubi wakati akizindua ugawaji wa chanjo ya hiyo leo Ijumaa, Julai 30, 2021 katika Bohari ya dawa MSD.

“Serikali kupitia mamlaka ya dawa na vifaa tiba (TMDA), Maabara ya Mkemia Mkuu, Maabara kuu ya Taifa, na vyombo vingine, vyote vimehakiki na kujiridhisha usalama na ubora wa hizi chanjo za Janssen kutoka kampuni ya Johnson & Johnson nchini Marekani,” amesema Profesa Makubi.

Amesema kutokana na mwongozo wa chanjo wa taifa dhidi ya Covid-19, Shirika la Afya Duniani (WHO), maelekezo ya COVAX FACILITY na upungufu wa uzalishaji wa chanjo toka viwandani, chanjo hizo kwa sasa zinatolewa kwa kufuata vipaumbele vya makundi yenye uhitaji mkubwa.

“Tumelenga ambayo watumishi wa sekta ya afya, watu wazima umri wa miaka 50 na kuendelea na watu wenye magonjwa sugu. Kama ambavyo Serikali imekuwa ikieleza, uchanjaji kwa makundi yote nchini ni wa hiari au huru,” amesema.

Profesa Makubi amesema kwa kuwa chanjo zilizopokelewa kwa sasa hazitoshelezi walengwa wa makundi yote nchini, makundi mengine yatapata chanjo katika awamu inayofuata, mara zitakapowasili.

Amesema Serikali inategemea kutoa chanjo kwa makundi yanayolengwa kuanzia Agosti 3, 2021, katika vituo 550 vya kutolea huduma katika mikoa yote ambapo orodha ya vituo hivyo inapatikana pia katika tovuti ya wizara; www.moh.go.tz.  

Kaimu Mkurugenzi Mkuu MSD, Benjamin Hubila amesema tayari kwa mkoa wa Dar es Salaam wameshasambaza chanjo 3400 ziliwemo zile zilizotolewa siku ya uzinduzi.
“Chanjo hizi tutasambaza katika mikoa 26 na ndani ya siku chache chanjo zote 1058400.


Tayari zitakuwa zimesambazwa na tutazingatia maeneo yenye maambukizi kuacha chanjo nyingi kama ambavyo tumepokea malekezo kwahiyo tutaacha 1000 mpaka 3000,” amesema.