Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cleopa Msuya: Kauli ya kila mtu atabeba msalaba wake iliniletea shida

Cleopa Msuya: Kauli ya kila mtu atabeba msalaba wake iliniletea shida

Muktasari:

  • Waziri Mkuu wa zamani, Cleopa Msuya amezungumza katika mahojiano maalum na Mwananchi kuwa kauli yake ya  ‘kila mtu atabeba msalaba wake’ aliyoitoa alipokuwa Waziri wa Fedha katika Serikali ya awamu ya pili baada ya wabunge kulalamikia hali ngumu ya fedha nchini,  ilimletea shida lakini ilikuja kueleweka kwa wananchi.

Dar es Salaam. Waziri Mkuu wa zamani Cleopa Msuya amesema kati ya mambo anayakumbuka katika utumishi wake serikalini ni pale alipowaambia Watanzania kuwa kila mtu atabeba msalaba wake.

Katika mahojiano hayo yaliyofanyika jana Jumatatu Aprili 19, 2021, Msuya aliyekuwa Waziri Mkuu mwaka 1980 hadi 1983 na 1994 hadi 1995,  amesema kauli hiyo aliyoitoa akiwa Waziri wa Fedha iliyeyuka yenyewe kwa majadiliano ya wananchi.

“Moja ya kauli ambayo nilikuwa quoted out of context (nje ya muktadha) na ikajirekebisha yenyewe, ilikuwa ni wakati wa bajeti. Tukawa tunajadili hapo Karimjee (Dar es Salaam). Sasa wabunge wengi wakawa wanasema ‘ooh mimi nimeona mke, mwingine nimeoa wake wawili, sasa itakuwaje’.”

 “Ikafika mahali mimi nikasema, kila mtu atabeba msalaba wake, kwa sababu haiwezekani mtu ukaamua kuoa wake wawili, sasa Serikali inataka kujenga shule watoto wasome halafu wewe unakuja unasema umeoa wake wawili? Kila mtu atabeba msalaba wake mwenyewe,” amesisitiza.

Amebainisha kuwa kauli hiyo ilizua mjadala mkali uliompa shida, ikabidi ajisalimishe kwa Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi.

“Nimelisema jioni pale, asubuhi wakati huo Rais alikuwa Mwinyi, nikamfuata nikamwambia, nimesema maneno hapa inawezekana yakakuletea matatizo. Mwinyi akasema wala usiwe na wasiwasi, haya mambo ni lazima tuwaelimishe watu wajue matokeo ya uamuzi wao.”

Amesema baada ya muda mjadala ulizidi kukolea kwa wananchi, lakini wakawa wakijibizana wenyewe kwa wenyewe mpaka kauli ile ikayeyuka.

Msuya  alipoulizwa kuhusu kauli yake nyingine iliyoibua mjadala ya kuwataka Watanzania kufunga mikanda, amesema alieleza ukweli wa hali iliyokuwepo.

“Hapo nilikuwa Waziri wa Fedha, niliwaambia wananchi wafunge mikanda. Kama kiongozi unaona hali siyo sawa unawaonya wananchi kwamba kuna hali inayoendelea huko chini ili wasilalamike,” amesema.