Dk Bashiru: Magufuli atamaliza muda wake akapumzike kama wenzake - VIDEO

Muktasari:

  • Baada ya taarifa mbalimbali ambazo zimekuwa zikisambaa kwa njia tofauti hususani mitandaoni zikieleza kuwa upo uwezekano wa Rais wa Tanzania, John Magufuli kuongeza muda wa kuongoza, Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amesema taarifa hizo hazina ukweli wowote

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amesema Rais wa Tanzania, John Magufuli hana mpango wa kubadilisha Katiba ili kuendelea kukaa madarakani kwa awamu ya tatu na wanaosema hilo watafute mtu mwingine wa kufanya hayo.

Dk Bashiru amesema hayo leo wakati akizungumza katika mahojiano maalum na Mwananchi ambapo amesema kuwa suala hilo limekuwa likizungumzwa kila siku lakini halina ukweli na hajui ni watu gani wamekuwa wakizusha taarifa hizo.

“Rais Magufuli ni mtiifu wa katiba ya chama na ya nchi, ni muaminifu kwa misingi ya kuasisiwa kwa Taifa hili na chama anachokiongoza, hatabadilisha kama watu wana mpango huo wapange kwa mtu mwingine sio Magufuli, atamaliza muda wake Mungu akimjalia na atarudi nyumbani kwake na wajukuu zake na shughuli zake kuungana na wenzake waliomtangulia kina mzee Mwinyi, mzee Mkapa na Kikwete

Dk Bashiru amesema Rais magufuli ameshasema na amekuwa akisema kwa ukali kuwa hataongeza muda na anashangaa kwa nini watu hawamuelewi huku akisema anamshukuru Rais mstaafu Benjamin Mkapa kwa kuwa na yeye alilisisitiza jambo hilo mkoani Mwanza huenda Watanzania wakamuelewa.

SOMA ZAIDI: