Luteni Urio: Sikuona umuhimu kurekodi mazungumzo yangu na Mbowe
Muktasari:
- Shahidi wa 12 Luteni Denis Urio amesema hakuona umuhimu kurekodi mazungumzo yake na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe baada ya kuulizwa na mmoja wa mawakili wa utetezi kwa nini hakufanya hivyo
Dar es Salaam. Shahidi wa 12 Luteni Denis Urio amesema hakuona umuhimu kurekodi mazungumzo yake na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe baada ya kuulizwa na mmoja wa mawakili wa utetezi kwa nini hakufanya hivyo
Shahidi huyo wa Jamhuri katika kesi ya ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzake watatu amesema hayo leo Alhamisi Januari 27, 2022 alipokuwa akiulizwa maswali na wakili wa utetezi Nashon Nkungu.
Soma maswali ya mawakili wa utetezi na majibu ya shahidi
Mahakama imerejea kwa ajili ya Jaji Joachim Tiganga kutoa uwamuzi baada ya Wakili wa utetezi Nashon Nkungu kuiomba Mahakama hiyo kutoa maelekezo kwa Shahidi wa 12 Luteni Denis Urio kujibu baadhi ya maswali ambayo alisema hawezi kuyajibu kutokana na kiapo chake cha kazi.
Baada ya Wakili Nkungu kuiomba mahakama kutoa maelekezo kwa shahidi kujibu maswali Jambo hilo liliibua mvutano wa kisheria uliosababisha Jaji Tiganga kuahirisha mahakama kwa muda kwa ajili ya kwenda kupitia vifungu mbalimbali vya sheria.
Tayari Mawakili wa pande zote wamejitambulisha, kutokana na kolamu zao kutobaadilika pande zote ziko tayari kwa uwamuzi.
Jaji ameanza kusoma uwamuzi kwa kupitia hoja zilizowasilishwa na pande zote
Jaji: Mahakama imekubaliana na maombi ya upande wa utetezi na kuelekeza Wakili anapomuuliza swali shahidi kulenga mambo yanayomuhusu Shahidi binafsi.
Wakili Nashon: Shahidi unakumbuka swali nililokuuliza?
Shahidi: Sikumbuki
Wakili Nashon: Nimekuuliza Levo yako ya ukomandoo
Shahidi: Mheshimiwa Jaji naomba nimpigie muajiri wangu simu kwanza
Jaji: Utakapoulizwa sema mahakama imenitaka nijibu
Shahidi: Nina Advance diploma ya parachuti
Wakili Nashon: Unaweza kukumbuka askari waliokuwepo kwenye mishe I Sudani 2011
Shahidi: Siwezi kukumbuka
Wakili Nashon: Na idadi ya askari waliokuwepo
Shahidi: Siwezi kukumbuka
Wakili Nashon: Na kwa Mwaka 2019
Shahidi: Siwezi kukumbuka
Wakili Nashon: Wakati Halfani Bwire alifukuzwa hukuwepo Tanzania
Shahidi: Ni sahihi
Wakili Nashon: Nawakati Ling'wenya anafukuzwa hukuwepo
Shahidi: Ni sahihi
Wakili Nashon: Nitakuwa sahihi ulikuwa na nia ovu kuzungumzia matukio ya hawa washtakiwa wakati hukuwepo
Shahidi: Sio sahihi
Wakili Nashon: Ni sahihi hufahamu kwa undani suala lililowafanya kufukuzwa kazi
Shahidi: Utovu wa nidhamu
Wakili Nashon: Utovu wa nidhamu sio kosa ila ndani yakee ndio kosa
Shahidi: Ni sahihi
Wakili Nashon: Kwahiyo hufahamu Halfan Bwire alifukuzwa kwa kosa gani
Shahidi: Sio jukumu langu
Wakili Nashon: Hujataja hatua wa makosa yaliyosababisha wao kufukuzwa
Shahidi: Sijata
Wakili Nashon: Hujataja aliyewafukuza
Shahidi: Sifahamu.
Wakili Nashon: Huwezi kufahamu siku na tarehe waliofukuzwa
Shahidi: Sifahamu
Wakili Nashon: Ni kweli hukutaja jina la huyo admin Ofisa aliyeekupa hizo taarifa.
Shahidi: Sikutaja
Wakili Nashon: Ni sahihi hukusema aliyekupa taarifa ni zaidi ya Admin Ofisa mmoja
Shahidi: Nilienda ofisini na kupitia mafaili na sio mtu aliyenipa taarifa.
Wakili Nashon: Huwezi kuiambia mahakama hawa walifukuzwa kazi kama hujataja aliyewafukuza
Shahidi: Waliofukuzwa na muajiri wao
Wakili Nashon: Unakumbuka siku mliyokutana na Freeman Mbowe Mikocheni
Shahidi: Ndio
Wakili Nashon: Wakati anakueleza mipango yake ulikuwa na akili timamu?
Shahidi: Ndio
Wakili Nashon: Muda huo ulikuwa hujawasilia na chombo chochote cha ulinzi
Shahidi: Ilikuwa bado
Wakili Nashon: Ni kisema kile kikao na wewe ulikaa kikao cha ugaidi utakubali
Shahidi: Sio sahihi
Wakili Nashon: Ni sahihi baada ya kile kikao ulikubali kwenda kumtafutia watu kutokana na ulikuwa na uchu wa madaraka
Shahidi: Sio sahihi sikuomba cheo
Wakili Nashon: Ni sahihi jeshi kuna kitu kinaitwa chini of information
Shahidi: Ni sahihi
Wakili Nashon: Inahusisha kutembea kwa taarifa
Shahidi: Hatutegemei taarifa
Wakili Nashon: Mgulani ni kambi ya jeshi?
Shahidi: Ni rest za jeshi
Wakili Nashon: Unapopata taarifa ni lazima upeleke kwa information officer
Shahidi: Sio lazima
Wakili Nashon: Wewe askari unapopata taarifa hutakiwi kupeleka kwa intelligence offers
Shahidi: Naomba kutoa maelezo unapopata taarifa kama hizi unatoa taarifa za haraka
Wakili Nashon: Jambo nyeti kama hili unakumbuka tarehe
Shahidi: Tarehe sikumbuki
Wakili Nashon: Ni muhimu unapoenda kwenye Ofisi za umma kujiandikisha
Shahidi: Sikujuandikisha nlitoa kitambulisho wakanitambua
Wakili Nashon: Ulisema Mbowe alisema anataka kuchukua dola
Shahidi: Ni sahihi
Wakili Nashon: Bila hata uchaguzi
Wakili Nashon: Alisema kwa kukata miti
Shahidi: Ili kuleta taharuki
Wakili Nashon: Mbowe angetaka kuchukua nchi ni kuchukua wanajeshi waliofukuzwa au kuchukua walioko kazini
Wakili Chavula: Naomba hilo lisiingie kwa kuwa anatafuta maoni ya shahidi.
Soma zaidi:Kesi ya kina Mbowe kuanza kesho kwa uamuzi
Wakili Nashon: Baada ya makubaliano yale ulimtafuta Bwire na kumueleza kuwa Mbowe anatafuta walinzi
Shahidi: Ni sahihi
Wakili Nashon: Na moyoni ukiwa unafahamu Mbowe anaenda kufanya ugaidi ukaniambia Bwire kuwa Mbowe anatafu mlinzi
Shahidi: Ni sahihi
Wakili Nashon: Na ukafanya hivyo kwa mshtakiwa wa kwanza na wa pili
Shahidi: Ni sahihi
Wakili Nashon: Kwa hiyo uliwadanganya washtakiwa
Shahidi. Sukudanganya niliwaambia
Wakili Nashon: Ulisema ulikutana na mshtakiwa wa kwanza wa pili na watatu Morogoro
Shahidi: Ni sahihi.
Wakili Nashon: Hebu isaidie mahakama kama unafahamu muda mwingine wowote mshtakiwa wa kwanza hadi wa nne walikutana Morogoro kula njama hizo
Shahidi: Sifahamu
Wakili Nashon: Vipi kuhusu na Moshi Aishi hoteli
Shahidi: Sifahamu
Wakili Nashon: Na Arusha
Shahidi: Sifahamu
Wakili Nashon: 2012 ulikuwa na renki gani
Shahidi: Koplo.
Wakili Nashon: Na ulivyokutana na Mbowe ulimwambia huna renk yoyote
Shahidi: Ni sahihi
Wakili Nashon: Jibu ulilompa lilikuwa ni sahihi
Shahidi: Kwangu mimi lilikuwa sahihi
Wakili Nashon: Ulisema hufungamani na chama chochote isipokuwa Kiongozi alioko madarakani
Shahidi: Ni sahihi
Wakili Nashon: Kwa hiyo ni ushahidi wako hukusema ni Kiongozi gani Rais au Mkuu wa Wilaya
Shahidi: Nilisema naheshimu mamlaka zilizoko madarakani
Wakili Nashon: Ulikuwa ukiwasiliana na Mbowe kwa njia ya simu
Shahidi: Ni sahihi
Wakili Nashon: Ulipoenda kwa DCI ulipewa mpelelezi gani
Shahidi: Kingai
Wakili Nashon: Wakati unawapa taarifa Kingai na DCI uliwaambia Mawasiliano yenu makubwa ni kwa njia ya simu
Shahidi: Niliwaambia
Wakili Nashon: Na wewe umewasilisha simu zako nne hapa mahakamani
Shahidi: Ni sahihi
Wakili Nashon: Hapakuwa na umuhimu wa kurekodi wakati wote mnaongea
Shahidi: Sikuona umuhimu
Wakili Nashon: Unaweza kueleza meseji hata moja kati ya ulizosoma yenye muelekeo wa ugaidi
Shahidi: Mtu mbili au tatu wanahitajika haraka ni meseji ya kwanza.
Wakili Nashon: Naomba kupatiwa kielezo namba 23. Shahidi naomba nitafutie meseji yenye kupanga ugaidi msomee Jaji.
Shahidi: Kaka zile mtu mbili au tatu zinahitajika ni muhimu siku zimeisha.
Wakili Nashon: Hiyo ndio uliona ya kupanga ugaidi
Shahidi: Kwa sababu walihitajika kwa kazi yao.
Wakili Nashon: Hakuna sehemu mlitumiana kwa ajili ya mishahara.
Shahidi: Ipo
Shahidi: Niwezeshe niweze kumobilaiz nikutane nao Morongo.
Wakili Nashon: Ni watu gani hao?
Shahidi: Sio magaidi
Mahakama. Kicheko…
Wakili Nashon: Ni sahihi ulimwambia Bwire kazi ikibadilika akupigie simu na alikupigia ni sahihi?
Shahidi: Mimi ndio nilimpigia.
Wakili Nashon: Ni lini alikupigia?
Wakili Nashon: Na ni sahihi Bwire kukupiga lilikuwa jambo jema
Shahidi: Ni sahihi
Wakili Nashon: Ulirudisha taarifa kwa Kingai kuwa Bwire amekupigia?
Shahidi: Ni sahihi
Wakili Nashon: Ulishangaa Bwire kukamatwa
Shahidi: Sikushangaa
Wakili Nashon: Kosa la Bwire liko wapi?
Shahidi: Sijui
Wakili wa utetezi John Malya kwa ajili ya mshtakiwa wa pili.
Wakili Mallya: Hizi meseji zinafanana na zile ulizokuwa unasoma?
Shahidi: Ndio
Wakili Mallya: Wapi alipokuita Home boy
Shahidi: Hakuna
Wakili Mallya: Ulimrekodi sauti wakati anakuta home boy
Shahidi: Hakuna
Wakili Mallya: Kwahiyo wewe ndio unajipendekeza kwa Mbowe, ni ushahidi gani ulioleta mahakamani
Shahidi: Ndio anavyoniitaga
Wakili Mallya: Kuna muamala wa tarehe 22/7/2020 una onyesha umetumiwa 199, 000 ulitumiwa kwenye namba 0787555200 ulipokea kutoka kwa nani?
Shahidi: Sikumbuki
Wakili Mallya: Inaonekana ilituma 190, 000 kwa Godson Mmari na baadae ukatuma 7,000 kwenye namba 0787000017 je mmoja ya watuhumiwa?
Shahidi: Hapana
Wakili Mallya: Ni sahihi hii fedha uliyotoa kwa Wakala ni 122,000 na wewe ulisema ulitoa Sh ngapi kwa Wakala?
Shahidi: Nilitoa 300, 000 kutoka mfukoni mwangu nikawapa
Wakili Mallya: Unakumbuka pale kwenye ule mgahawa mlikula
Shahidi: Ni sahihi
Wakili Mallya: Nani alilipa
Shahidi: Mimi
Wakili Mallya: Ulitoa wapi fedha za kuwalipia
Shahidi: Ni hela za Freeman Mbowe
Wakili Mallya: Uliomba hela za nini
Shahidi: Za kuwasafirisha
Wakili Mallya: Kuna sehemu ambayo Mbowe alikwambia anakupa pesa ya kuwapa chakula?
Wakili Mallya: Ila wewe ukaona uwalishe magaidi
Wakili Mallya: Kuna neno chakula hapo umelitoa wapi?
Shahidi: Hapana
Shahidi: Nilikuta wanakula na mimi nikajiunga kula, kisha nikalipa
Wakili Mallya: Twende Kwenye mhamala wa Sh500,000
Wakili Mallya: Nani alikutumia hii pesa
Shahidi: Freeman Mbowe
Wakili Mallya: Ulitoa Sh300,000
Wakili Mallya: Ulielezea Mahakama Kwamba Sh200,000 ulimpa nani?
Shahidi: Nilimpa Adamoo na Ling'wenya
Wakili Mallya: Kuna sehemu umesema kwamba ulitoa Sh ngapi?
Shahidi: Nilikuwa na Cash Mfukoni
Wakili Mallya: Wakati unaaongozwa na wakili ulisema kuna fedha ulizotoa mfukoni ukawapa washtakiwa?
Shahidi: Sikuulizwa
Wakili Mallya: Ulisema baada ya vijana wanne kufika kwa Mbowe alikuwa hakupi tena ushirikiano
Shahidi: Ni sahihi
Wakili Mallya: Ni sahihi siku unayoenda kumuona alikuwa anatembea na magongo
Shahidi: Sikumuona ilikuwa usiku lakini aliniambia amepigwa na wahuni
Wakili Mallya: Na Unafahamu alikuwa anauguliwa na mtoto
Shahidi: Sifahamu
Wakili Mallya: Unafahamu mwaka jana kulikuwa na uchaguzi mkuu
Shahidi: Ni sahihi
Wakili Mallya: Kutoka tarehe 20/7,2020 hadi Octoba wakati wa uchaguzi kulikuwa na miezi mitatu ifike uchaguzi
Shahidi: Ni sahihi
Wakili Mallya: Wakati wa uchaguzi unajua huwa kuna vurugu
Shahidi: Za kawaida
Wakili Mallya: Mtu kuwa na walinzi ni kosa?
Shahidi:Kuwa na mlinzi sijui kama ni kosa au kosa
Wakili Mallya: Umempa mtu hela umemwambia nenda kwa Mbowe ukawe mlinzi ni kosa?
Shahidi: Kwa wakati huo sio kosa
Wakili Mallya: Hao mtu tatu au nne uliwaambia wakafanye nini
Shahidi: Shahidi Kuambatana kazi ya Ulinzi
Wakili Mallya: Nionyeshe kwenye meseji mahali Mbowe anasema anaenda kuvunja Sheria
Shahidi: Hakuna
Wakili Mallya: Ilikuwa una wajibu wa kuwasaidia polisi kukusanya ushahidi ili uhalifu wa Mbowe ufahamike
Shahidi: Ni sahihi
Wakili Mallya: Nisomee meseji hii
Shahidi: Usiwe unatumia namba yako kutuma pesa tumia wasaidizi wako au Wakala
Wakili Mallya: Umemuelekeza Mbowe cha Kufanya, ni sahihi akitekeleza unachosema haitoonekana namba yake
Shahidi: Ni sahihi
Wakili Mallya: Ni swali langu la mwisho kwa jioni hii
Mheshimiwa Jaji muda umetutupa mkono naomba ahirisho hadi kesho nitakapoendelea na maswali kwa shahidi kwa niaba ya mshtakiwa wa pili.
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Hatuna pingamizi Mheshimiwa Jaji.
Jaji: Kutokana na muda na kufuatia maombi ya Wakili wa utetezi John Mallya naahirisha kesi hii hadi kesho Januari 28, 2022 saa tatu asubuhi kwa ajili ya shahidi wa 12 kuendelea kuhojiwa na upande wa utetezi.