Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabala: Walimu wapewe posho mazingira magumu

Muktasari:

  • Wadau wameshauri posho ya vikao wanayopewa wabunge zitolewe kwa walimu ili kuwapa moyo wa kufundisha na kukuza elimu nchini.

Dar es Salaam. Wadau wa elimu wameshauri walimu kupewa motisha ikiwemo posho kwa wanaoishi katika mazingira magumu, ili kuwapa ari ya kufundisha na kukuza elimu nchini.

Wameyasema hayo leo katika mjadala wa Mwananchi Twitter Space leo Jumatano Januari 11, 2023 unaoangazia ‘kipi kifanyike ongezeko la uandikishaji darasa la kwanza na kidato cha kwanza, liendane na utoaji wa elimu bora nchini’.

Akichangia mjadala huo, Ashura Kayupayupa ameshauri posho ambayo wamekuwa wakipewa wabunge ni vema wakapewa walimu ili kutoa motisha zaidi kwa kundi hilo.


“Kama wabunge wanapewa sitting allowance kwa nini hili halifanyiki kwa walimu licha ya mishahara yao kuwa midogo?” amehoji Kayupayupa.

Amesema ni ngumu kuongeza idadi ya wanaojiunga shule bila kuboresha ubora wa huduma unayoitoa hayo ni matumizi mabaya ya rasilimali muda.

Kwa upande wake Mwalimu na mtunzi wa vitabu, Richard Mabala ameishauri Serikali kuangalia namna ya kutoa motisha kwa walimu ikiwemo posho kwa wanaoishi katika mazingira magumu badala ya kuwashurutisha kwenda vijijini.

“Kuna mengi ya kuyarekebisha, badala ya kushurutisha walimu kwenda vijijini tutafute motisha ya walimu kwenda huko, Serikali inaweza kuweka posho ya kuishi katika mazingira magumu ili waweze kufanya kazi katika mazingira hayo,” amesema.

Amesema ni muhimu kusikiliza sauti ya walimu, kuna chama cha walimu lakini wengi hawaoni kama chama hicho kinapigania maslahi ya walimu.

Mabala amesema mwalimu anaweza kufundisha bila darasa lakini darasa haliwezi kufanya kitu chochote bila mwalimu.

“Badala ya kuweka madarasa mengi nguvu kubwa sasa iwekwe kwa walimu ili kuwe na uwiano kati yao na wanafunzi na madarasa.

“Nchi zilizofanikiwa kwenye elimu kama Finland au Singapore wamewekeza zaidi kwenye elimu na kuhakikisha wale waliofaulu vizuri wanaingia kwenye sekta ya elimu,” amesema.

Kayupayupa ameongeza kuwa tatizo lingine ni lugha ya kufindishia ambayo watoto hawailewi na si wao tu hata walimu pia hawaielewi.

Mbunge wa Viti Maalum, Nusrat Hanje amesema ni vigumu kwa walimu kufundisha lugha ambayo hawaijui na wanafunzi wakaielewa.

“Mjadala wa lugha gani tutumie ni muhimu sana hii ni nchi yetu na viongozi wanatoa dira kama una elimu ambayo haitafsiriki tunataka kwenda wapi? Lazima tujadili elimu tunayoihitaji ijapokuwa kuna vitu vimefanyika lakini kuna vitu vya msingi bado vinafanywa kama vya ziada ambavyo huenda ndivyo kwa msingi,” amesema Hanje.