Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mahita aanza kutoa ushahidi kesi ndogo ndani ya kesi kubwa ya Mbowe

Mahita aanza kutoa ushahidi kesi ndogo ndani ya kesi kubwa ya Mbowe

Muktasari:

  • Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imeanza kupokea ushahidi kwa Mkaguzi wa Jeshi la Polisi, Mahita Omary Mahita katika kesi ndogo ndani ya kesi kubwa ya msingi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.


Dar es Salaam. Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imeanza kupokea ushahidi kwa Mkaguzi wa Jeshi la Polisi, Mahita Omary Mahita katika kesi ndogo ndani ya kesi kubwa ya msingi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Mahita anatoa ushahidi wake leo Ijumaa Septemba 17, 2021, kuthibitisha kielelezo (maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa pili) kilichowasilishwa mahakamani hapo na upande wa mashtaka kilikuwa ni sahihi.

Septemba 15, 2021 upande wa utetezi walipinga maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo Adam Kasekwa yasipokelewe na mahakama hiyo kwa sababu yalichukuliwa nje ya muda wa kisheria na mshtakiwa huyo anadai kuwa aliteswa wakati anaandika maelezo yake kituo Kikuu Cha Polisi Dar es Salaam.

shahidi huyo anaongozwa kutoa ushahidi wake na wakili wa Serikali Mwandamizi, Pius Hilla, mbele ya Jaji Mustapha Siyani.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi