Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majaliwa akabidhi pikipiki 49

Muktasari:

Waziri Mkuu amewataka vijana waendesha pikipiki kuzitimua pikipiki alizowapa ili ziwe na tija kwa maisha yao na kuwataka watii sheria za barabarani ikiwamo kuvaa kofia ngumu na kutobeba abiria zaidi ya mmoja.

Ruangwa. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekabidhi pikipiki 49 kwa vijana wa wilaya ya Ruangwa ili waweze kujiajiri na kujikwamua kiuchumi.

Waziri Mkuu amekabidhi pikipiki hizo leo baada ya kumaliza kuhutubia wananchi kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Likangara. 

Amewataka vijana hao kuhakikisha wanakuwa waaminifu kwa kufanya kazi kwa bidii ili pikipiki hizo ziwe na tija.

Amesema vijana wanaoendesha pikipiki maarufu bodaboda wanatakiwa kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali.

“Ukiendesha pikipiki lazima uhakikishe kwamba una leseni, bima, vaa kofia ngumu wewe na abiria wako na marufuku kubeba abiria zaidi ya mmoja.”Amesema

Wakizungumza baada ya kukabidhiwa pikipiki hizo vijana hao ambao walikuwa wakiendesha pikipiki za watu, wameahidi kufanya kazi kwa bidii.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika Zahanati ya Nandagala na kuridhishwa na maendeleo yake.

Amesema kukamilika kwa majengo hayo kutarahisisha upatikanaji wa haraka wa huduma za afya kwa mama na mtoto. Pia itawapunguzia kutembea umbali mrefu kwenda kufuata huduma hizo katika hospitali ya wilaya ya Ruangwa.