Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majaliwa kufungua mkutano mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania

Mjumbe wa kamati tendaji jukwaa la Wahariri Tanzania, Neville Meena akifafanua jambo kwa Waandishi wahabari (hawapo pichani). Picha na Bahati Mwatesa

Muktasari:

  • Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa anatarajiwa kufungua Mkutano Mkuu saba wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kesho Jumatatu, Novemba 12, 2023 mkoani Lindi.

Lindi. Mkutano Mkuu wa saba wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) unatarajiwa kuanzia kesho Jumatatu Novemba 13-15, 2023, mkoani Lindi.

Mkutano huo wenye kauli mbiu ‘Uandishi wa Habari, Gesi na Uchumi Endelevu’ utafanyikia Uwanja wa Ilulu, mkoani Lindi na kufunguliwa na Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

Akizungumza na waandishi wa habari, leo Jumapili, Novemba 12, 2023, Mjumbe wa Kamati Tendaji ya TEF, Neville Meena amesema, mkutano huo wameamua kuufanyia mkoani Lindi kwa sababu, mkoa huo una mradi mkubwa wa gesi ambayo utakuja kuongeza pato la Taifa.

Meena amesema mradi wa gesi utafungua fursa nyingi za uwekezaji na ndio maana wameamua kwenda kufanya mkutano huo mkoani humo.

Amesema mkutano huo utahudhuriwa na washiriki mbalimbali zaidi ya 120 kutoka ndani na nje ya nchi zikiwemo Kenya na Uganda.

"Tumekuja kufanya mkoani Lindi kwa sababu Mkoa wa Lindi una fursa ya mradi mkubwa wagesi asilia, kwahiyo kuja kufanyia huku ni kuhakikisha tunautangaza Mkoa wa Lindi kupitia mkutano wetu kwani watu wengi wanakuja kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Kenya na Uganda,” amesema Meena

"Kwanini tumekuja kufanyia Lindi, ni sehemu ya Tanzania, miaka michache ijayo patakuwa na mradi mkubwa wa LNG, huwezi kuwatenganisha waandishi wa habari na mradi huu mkubwa utakao kwenda kuongeza pato la taifa kwa miaka ijayo,” amesema

Amesema mkutano huo utahudhuriwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, Novemba 14, 2023.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Lindi (LPC), Fatuma Maumba amesema kufanyikia mkutano huo mkoani humo kutasaidia kwa kiwango kikubwa kama wanahabari kujifunza mambo mbalimbali ambayo inawezekana kwa kiasi kikubwa kama wanahabari hawakuwa wanayafahamu.

"Mkutano huu utatufungulia fursa mbalimbali na kujifunza mambo mengi ambayo kama wanahabari tulikuwa hatuyafahamu. Pia kuja kwa watu kutoka nchi zingine ni fursa kubwa sana kwa mkoa wa Lindi na ukizingatia hapa kwetu Lindi tuna mradi mkubwa wa gesi,” asema Fatuma ambaye pia ni Mwandishi wa Habari wa ITV.