Majaliwa: tutafuatilia fedha zote za maendeleo

Muktasari:

  • Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali haitalega hata kidogo kufuatilia matumizi ya fedha za  miradi ya maendeleo ili kujiridhisha na ubora wa miradi husika.

Dar es Salaam. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali haitalega hata kidogo kufuatilia matumizi ya fedha za  miradi ya maendeleo ili kujiridhisha na ubora wa miradi husika.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo Jumapili, Oktoba 10,2021 jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa kampeni ya maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko-19.

Amesema kazi za utoaji wa huduma kwa jamii zinazoendelea nchi nzima, ikiwemo kwenye sekta ya elimu, afya, maji na kilimo Mawaziri kwa kushirikiana na Makatibu Wakuu, wakuu wa mikoa wanaendelea kuisimamia.

“Kama alivyosema Waziri wa Fedha na Mipango, tutaendelea kutoa fedha kwaajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo, mimi na mawaziri wenzangu kwa kushirikiana na wakuu wa mikoa kutoka pande zote mbili za muungano, nikuhakikishie mheshimiwa Rais kiwango chochote cha fedha utakachokitoa tutakifuatilia pale kilipopelekwa na matumizi yake,”amesema Majaliwa.

“Kama tunavyowasikia viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanavyosema, tangu umeingia madarakani wanakauli yao wanasema, umeupiga mwingi kazi nzuri ulioifanya watanzania wameiona tutahakikisha malengo yako yanafika hadi vijijini,”