Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mlinzi auawa Chato akiwa lindo, apigwa na kitu kizito

Nyumba ya kulala wageni ya Kings iliyopo Buseresere Wilayani Chato mkoani Geita alikokuwa akilinda Mashaka wakati wa uhai wake.

Muktasari:

  • Mlinzi binafsi katika nyumba ya kulala wageni ya Kings iliyopo mji mdogo wa Buseresere Wilayani Chato mkoani Geita ameuawa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali shingoni na kichwani.

Geita. Mtu mmoja aliyetambuliwa kwa jina moja la Mashaka, mkazi wa Buseresere wilaya ya Chato mkoani Geita ameuawa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali shingoni na kichwani na kusababisha kifo chake.

Mtu huyo alikuwa mlinzi katika nyumba ya kulala wageni ya Kings iliyopo mji mdogo wa Buseresere.

Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Katoro, Zakayo Sungura amekiri kuupokea mwili wa mlinzi huyo na kusema ulipelekwa na askari polisi asubuhi ya Jumamosi Februari 11, 2023 na kwamba mwili umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo ukisubiri taratibu za kipolisi na ndugu.

“Mwili ulikua na majeraha katika sehemu ya kichwani na shingoni na kifo chake kinaonyesha kimetokana na kuvuja damu nyingi. Jeraha lake linaonyesha amepigwa na kitu chenye ncha kali,” amesema Sungura.

Mwenyekiti wa kijiji cha Buseresere, Deus Manga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema limetokea usiku wa kuamkia Februari 11, 2023 ambapo wauaji baada ya kutimiza azma yao waliondoka bila kuchukua mali yoyote.

“Asubuhi mlinzi kauawa, amepigwa na kitu kizito kwenye taya karibu na sikio, alikua ametokwa na damu nyingi. Watu walihisi amechinjwa lakini polisi ndio watatuambia baada ya uchunguzi alipigwa usiku hata wenye Guest hawakusikia, wafanyakazi walikua wamelala ndani na wao wametoka wakakuta mlinzi ameuawa,” amesema Manga.

“Hapa Kings kuna ngome, mlinzi huyu alikua ndani ya geti na hili geti huwa linafungwa kwa kufuli, tumekuta limekatwa na mkasi, wakaingia ndani, wakamuua lakini hawajachukua kitu chochote wala kufanya uharibifu wa mali,” amesema Manga.

Akizungumzia mauaji ya walinzi ambayo huripotiwa mara kwa mara mkoani hapa, Manga amesema ili kukomesha mauji haya Serikali kwa kushirikiana na jeshi la polisi wanapaswa kufanya uchunguzi wa kina kubaini wanaohusika na mauji hayo.

Mmoja wa wahudumu katika nyumba hiyo ya kulala wageni, Dativa Mathias amesema siku ya tukio aliamka saa 11 alfajiri na kwenda kwenye chumba alicholala bosi wake kwa lengo la kuchukua funguo lakini alipomwamsha hakuamka.

Amesema alitoka nje kumuomba mlinzi simu ili ampigie na alipofika alimkuta amelala chini huku shuka la kimasai analotumia likiwa hadi kichwani jambo ambalo sio kawaida.

“Nilipomkuta chini nilishtuka maana tumemzoea kama anataka kulala huu nganisha viti viwili lakini hii siku nilimkuta sehemu tofauti na amelala chini kabisa nikapata hofu nikarudi kumgongea bosi kwa sauti ndio akaamka tukatoka nje na kuwasha tochi ya simu mana alipokuwa palikuwa na giza kidogo ndio tukaona damu nyingi imetapakaa chini tukaita polisi,” amesema.

Mathias amesema wauaji hao hawakuchukua kitu chochote kwenye bar ya hoteli hiyo.

Usiku wa kuamkia Disemba 22, 2022 watu wasiojulikana waliwaua kwa kuwapiga na kitu kizito kichwani walinzi watatu wa kampuni binafsi wakati wakiwa lindo katika eneo la Mtaa wa Shilabela mjini Geita.

Matukio ya kuuawa kwa walinzi yamekuwa yakiripotiwa mara kwa mara na Serikali kulaani matukio hayo ambapo sasa wananchi wameomba ili kuyakomesha, Serikali iunde timu ya kuchunguza wanaohusika kwakuwa wauaji hao hawapori mali yoyote kwenye eneo la tukio.