Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ni rahisi kudhibiti udumavu wa watoto kwa kufanya haya

Daktari wa wanyama wa Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma David Msombe,  akiwachoma sindano ya kinga mbuzi kabla ya kugawiwa kwa makundi mbalimbali ya wanawake wilayani humo.

Muktasari:

Wakati kiwango cha udumavu nchini kikitajwa kuwa ni asilimia 30 Tanzania, vyakula vyenye asili ya wanyama vinatajwa na wataalam wa lishe kusaidia kukabiliana na hali hiyo kwa haraka zaidi kuliko vyakula vya jamii ya mikunde.

Chamwino. Changamoto ya vyakula vyenye asili ya wanyama inatajwa kuwa ni tatizo kubwa mkoani Dodoma, jambo ambalo linasababisha udumavu kwa watoto walio chini ya miaka mitatu.

Kwa mujibu wa utafiti wa Hali ya Uzazi ya Afya ya Mama na Mtoto na Malaria (TDHS) inaonesha kuwa hali ya udumavu imepungua nchini hadi asilimia 30 mwaka 2022 kutoka asilimia 31.8 mwaka 2018.


Meneja wa mradi wa Lishe Yangu Maisha Yangu unaoendeshwa na Shirika la Kulinda Watoto la Save the Children, Mariam Mwita amesema vyakula vya asili ya wanyama, ni muhimu katika kukuza mwili na akili kwa binadamu na hata ufyonzaji wake wa virutubisho ni asilimia 100.


Amesema kwa watoto wadogo ufanyanyaji wa kazi wa vyakula vya asili ya wanyama katika kuongeza virutubisho, ni mkubwa  ukilinganisha na vyakula vya jamii ya mikunde.


Amesema katika kukabiliana na changamoto hiyo, shirika hilo lilianzisha mradi wa Lishe Yangu Maisha Yangu ambao unalenga kutoa elimu ya lishe bora, ufugaji wa  mbuzi wa maziwa na uanzishaji wa bustani ya mboga mboga katika kaya.


 “Lengo la ugawaji wa mbuzi ni kusaidia kaya hizi ziweze kupata vyakula vya asili ya wanyama ambalo ndio tatizo kubwa sana kwa mkoa wa Dodoma ambalo ndio maana watoto wanadumaa kwa kukosa vyakula vyenye asili ya wanyama,”amesema Mariam ambaye pia kitaaluma ni bingwa wa lishe na afya ya jamii.


Amesema mradi huo wa miaka mitatu ulioanza Julai 2023 na utakaomalizika Juni 2026, utawanufaisha watu 6,231 moja kwa moja na wasio wa moja kwa moja zaidi 120,000 katika wilaya za Bahi na Chamwino.


Mmoja wa wanufaika wa mradi huo kutoka kijiji cha Chinene wilayani Chamwino, Nasra Mwanangela amesema baada ya kupata mafunzo kuhusu makundi matano ya vyakula na kuanza kutengeneza bustani ya mbogamboga, mtoto wake ambaye ongezeko la uzito lilikuwa likisuasua ameanza kuimarika.


“Kabla ya mradi huu mtoto alikuwa haongezeki uzito kabisa, anaenda hata miezi mitatu mfululizo kilo ni hizo hizo tisa alizokuwa nazo wakati akiwa na umri wa miaka miwili. Lakini baada ya mradi huu mtoto ameanza kuongezeka kwa gramu kati ya 500 hadi 600 kwa mwezi,” amesema.