Padri soka asomewa maelezo ya awali

Padri Sostenes Soka aliyejifunika na kofia ya sweta kichwani akiingia katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi kusomewa maelezo ya awali Katika shitaka linalomkabili la kubaka mtoto wa miaka 12

Muktasari:

Sostenes Bahati Soka, Padri wa Kanisa Katoliki, Parokia Teule ya Mtakatifu Deonis Aropagita, Jimbo la Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro leo Octoba 10,2022 amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi kusomewa maelezo ya awali Katika shitaka linalomkabili la kubaka mtoto wa miaka 12.

Moshi. Sostenes Bahati Soka, Padri wa Kanisa Katoliki, Parokia Teule ya Mtakatifu Deonis Aropagita, Jimbo la Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro leo Octoba 10,2022 amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi kusomewa maelezo ya awali Katika shitaka linalomkabili la kubaka mtoto wa miaka 12.

September 26, 2022 padri huyo alipandishwa kizimbani Katika mahakama hiyo na kusomewa mashitaka mawili katika mahakama ya Hakimu Mkazi, huku shitaka la tatu likifunguliwa katika mahakama ya wilaya.

Hata hivyo waandishi wa habari wamesubirishwa nje ya chumba cha mahakama hiyo, ambapo baada ya kuendeshwa kwa shauri hilo wakili wa Serikali atatoa ufafanizi juu ya yaliyojiri mahakamani hapo.