Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi Shinyanga wakamata silaha, vifaa vya wizi

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi

Muktasari:

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi, amesema vifaa hivyo wamevikamata wakati wakifanya msako wa kipindi cha Novemba 22 hadi Desemba 12 mwaka huu.

Shinyanga. Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, limekamata dawa za kulevya, bunduki, simu za mkononi, mitungi ya gesi, panga na mashoka vinavyodaiwa kutumika kutekeleza uhalifu.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya vifaa hivyo leo Desemba 19, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi, amesema vifaa hivyo wamevikamata wakati wakifanya msako wa kipindi cha Novemba 22 hadi Desemba 12 mwaka huu.

Magomi amesema katika msako huo wamekamata vifaa tiba vya zahanati ya Uyongo iliyopo katika Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama, bunduki moja aina ya gobore, simu za mkononi 17, pikipiki 10, dawa za kulevya heroine 10, bangi kete 71, runinga nne, mitungi ya gesi miwili na lita 20 za gongo.

Vitu vingine ni pamoja na vyuma vya ujenzi wa minara ya Tanesco, spika mbili, vitenge doti nne, kompyuta tatu, subwoofer nne, monita moja, godoro moja, panga moja, shoka moja, makabati mawili ya kuhifadhia chipsi, huku wakiokota pikipiki nane na baiskeli 11.

“Kutokana na kukamatwa kwa vifaa hivyo tunawaomba wananchi wa Mkoa wa Shinyanga wafike katika kituo kikuu cha polisi kwa ajili ya kuzitambua mali zao kuanzia Desemba 22 hadi 30,” amesema Magomi.

Pia katika kipindi cha mwaka huu, Polisi wamesema wamewafikisha watuhumiwa mahakamani na wameshatolewa hukumu, wakiwamo waliotuhumiwa kwa wabakaji waliojihusisha na vitendo vya ulawiti, kujeruhi, wizi wa mtoto na kumpa mimba mwanafunzi.

Aidha kesi zingine zilizotolewa ni hukumu za kupatikana na dawa za kulevya ikiwamo bangi na mirugi ambapo wahusika wamefungwa jela.