Rais Samia azindua mkakati uelimishaji na uhamasishaji Sensa

Tuesday September 14 2021
rais azinduapicc
By Elizabeth Edward

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amezindua mkakati wa uelimishaji na uhamasishaji wa sensa ya watu na makazi itakayofanyika 2022.

Akizungumza leo Jumanne Septemba 14, 2021 jijini Dodoma kabla ya kuzindua mkakati huo,  Rais Samia amesema sensa ni muhimu kwani inakwenda kusaidia utekelezaji wa mipango ya Serikali.

Amesema kwa kutambua idadi ya watu na shughuli wanazofanya inasaidia Serikali kujipanga vyema katika ugawaji wa rasilimali.

Kuhusu wanaobeza Serikali kutumia fedha kufanya zoezi hilo amesema ni muhimu kwa taifa kuwa na takwimu zake .

“Kumekuwa na hoja kwanini Tanzania itumie fedha hizo kwenye zoezi la sense, sababu ni kwamba kama tunaweza kufanya wenyewe na kupata idadi yetu kwanini tutumie namba zinazotolewa na vyombo vingine vya kimataifa,” amesema.

Soma zaidi: #Live Rais Samia kuzindua mkakati wa uelimishaji Sensa

Advertisement


Rais amesisitiza zoezi hilo lifanywe kwa ufanisi kwa maana ya muda na gharama nafuu, ikizingatiwa nchi bado inapambana kujinasua kwenye mtanziko wa kiuchumi uliosababishwa na janga la Uviko 19.

Advertisement