Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

RC Mtanda ataka mabadiliko Jiji la Mwanza, makazi duni kuondolewa

Muktasari:

  • Mtanda amewataka wataalamu wa ardhi kuachana na miradi aliyoiita kichefu chefu na kubuni miradi mikubwa ya makazi itakayoipa hadhi Jiji la Mwanza.

Mwanza. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda amewataka wataalamu wa sekta ya ardhi kuwa wabunifu na kuanzisha miradi mikubwa itakayobadilisha sura ya Jiji la Mwanza na kuondoa makazi duni yaliyopo katikati ya Jiji hilo.

Akizungumza leo Jumatano Julai 2, 2025 kwenye kikao cha tathmini ya utendaji kazi kwa wataalamu wa sekta ya ardhi mkoani humo, Mtanda amesema haiwezekani kati kati ya Jiji hilo kuwe na makazi duni, akiwataka wataalamu hao kuja na bunifu zitakazobadili hali hiyo badala ya kung’ang’ania miradi iliyobuniwa miaka mingi iliyopita bila tija.

“Tuwe na uwezo wa kuwa wabunifu katika mipango ikiwemo ya kuwa na miradi mikubwa. Hatuwezi kuendelea kukaa na slums (makazi duni) katikati ya jiji la Mwanza,”amesema Mtanda

Amewataka kuachana na miradi aliyoiita kichefu chefu ambayo baadhi wameikuta kutoka kwa watangulzi wao ambayo inawafanya wafokewe na kila kiongozi anayekwenda kutembelea miradi hiyo.

 “Umeukuta mradi wa miaka 20 iliyopita, miradi kichefu chefu kila kiongozi anayekuja anawafokeeni nyie haoni jambo jipya  lakini mkianzisha miradi mipya itatusaidia,”ameongeza.

Mtanda pia amesisitiza umuhimu wa kushughulikia migogoro ya ardhi kwa kushirikisha wananchi na viongozi wa mitaa ili kuepuka migogoro mipya.

“Tuendelee kushughulikia migogoro ya zamani bila kuibua mipya. Wapo baadhi ya watumishi wa ardhi wanaojulikana kwa kusababisha migogoro. Hili lazima likomeshwe,” ameonya.

Ameagiza kuendelezwa kwa utaratibu wa kliniki za ardhi angalau mara mbili kwa mwaka, akieleza kuwa kliniki hizo zinasaidia kutatua migogoro mingi ya ardhi.

Aidha, amewaonya wataalamu wa ardhi dhidi ya vitendo vya rushwa, akisema vinaathiri kwa kiwango kikubwa ufanisi wa kazi na kuwavunjia wananchi imani.

Awali akitoa taarifa kwa Mtanda, Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Mwanza, Wilson Luge amesema lengo la kikao hicho ni kufanya tathmini ya namna walivyotekeleza majukumu yao kwa mwaka 2024/25 pamoja na kujipanga namna bora ya kwenda kutekeleza majukumu yao mwaka mpya wa fedha 2025/26 ulioanza Julai Mosi.

Amesema kikao hicho kimehudhuriwa na wataalamu wa ardhi kutoka Halmashauri nane za Mkoa wa Mwanza, wakuu wa idara na maofisa mipango miji, wadau wa ardhi pamoja na makamishina wa ardhi wasaidizi kutoka baadhi ya mikoa ya Kanda ya Ziwa ukiwemo wa Simiyu, Mara na Kagera.

Amesema idara ya ardhi imeendelea kuboresha matumizi ya ardhi mkoani Mwanza kwa kupanga, kupima na kutoa hati likiwemo eneo la Busisi wilayani Sengerema ambapo Serikali imetoa zaidi ya Sh1 bilioni kuliboresha liendane na hadhi ya daraja la JP Magufuli.

“Tuna mpango wa kutoa ardhi katika eneo la Busisi ambapo tutapanga viwanja, kupima na wananchi watamilikishwa rasmi. Shughuli hili iitasaidia kuondoa ujenzi holela usioendana na hadhi ya daraja,” amesema Luge.

Amesema wapo wananchi waliopima ardhi, lakini wengi bado wanamiliki kimila na sasa ni muda wa kupandisha hadhi ya ardhi hiyo kwa kupanga matumizi rasmi  ikiwa ni pamoja na kuweka maeneo ya huduma kama vituo vya afya, stendi za daladala, hoteli za kitalii na barabara.