Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rotary Oysterbay kukusanya Sh320 milioni kuboresha afya, elimu

Rais wa Klabu ya Rotary ya Oysterbay, Abdulrahman Hussein (katikati) akizungumza na waandishi wa habari, kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Vodacom Foundation, Harriet Lwakatare (mwenye koti jekundu). Picha na George Helahela

Muktasari:

  • Klabu ya Rotary ya Oysterbay inatarajia kukusanya Sh320 milioni katika mashindano ya mbio za mbuzi kwa ajili ya kusaidia jamii katika sekta ya afya na elimu, mbio hizo zitafanyika Septemba 9, 2023

Dar es Salaam. Klabu ya Rotary ya Oysterbay inatarajia kukusanya Sh320 milioni katika mashindano ya mbio za mbuzi kwa ajili ya kusaidia jamii katika sekta ya afya na elimu.

Hayo yamesemwa na Rais wa klabu hiyo, Abdulrahman Hussein Ijumaa Agosti 25, 2023 akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mashindano hayo ya mwaka huu yanayotarajiwa kufanyika Septemba 9, 2023 katika Viwanja vya The Green, Oysterbay.

“Tunatarajia kukusanya wadau wa maendeleo zaidi ya 3,000 kwa ajili ya kushiriki mbio za mbuzi kwa lengo la kukusanya Sh320 milioni zitakazotumika kutoa msaada kwa jamii hususan katika sekta ya Elimu na Afya,”amesema Hussein.

Mbio hizo zilizoandaliwa na Klabu hiyo zinakuwa za nne kupewa jina la ‘Goat race’ huku wadhamini wakuu wakiwa Vodacom Tanzania.

“Katika mbio za mwaka huu tumepanga kukusanya fedha ambazo tutarudisha kwa jamii katika sekta ya elimu na afya kwani ndiko jamii inaweza kuwa na ustawi thabiti kama kukiwekewa nguvu, tumekuwa tukifanya hivyo miaka yote ila mwaka huu tutafanya kwa ukubwa,”amesema Hussein.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Vodacom Foundation, Harriet Lwakatare amesema wamedhamini mbio hizo kwa ajili ya kuchochea maendeleo jumuishi katika jami.

“Tunashiriki mbio hizi kwa sababu malengo ni kurudisha kwa jamii, nasi tunafanya hivyo ili kuwa na maendeleo jumuishi kwenye sekta tofauti nchini,”amesema Harriet.

Meneja wa miradi wa mbio hizo mwaka huu, Paul Muhato amesema mwaka jana walikusanya Sh246 milioni na walisaidia ujenzi wa vyoo mashuleni pamoja na ukarabati wa madarasa jijini Dar es Salaam huku mwaka huu wakijikita zaidi katika udhamini wa masomo ya juu.

“Mbio za 2022 fedha tulizokusanya zilisaidia katika ujenzi wa vyoo na ukarabati wa madarasa katika baadhi ya shule ya msingi jijini hapa lakini mwaka huu katika elimu tutajikita pia na udhamini kwa wanafunzi wa elimu ya juu wasio na uwezo kifedha,”amesema Muhato.

“Mbali na kukusanya fedha hizo lakini pia tuna lengo la kuikutanisha jamii pamoja na watu wenye uhitaji maalumu kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano na kusherehekea pamoja,”ameongeza Muhato.

Rotary Internation ni asasi yenye wanachama zaidi ya milioni 1.4 ambayo inashughulika na masuala ya kijamii na kwa Tanzania zipo klabu 37 za asasi hiyo huku kubwa ikiwa ya Oysterbay.