Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Samia ataka bandari itumike usafirishaji korosho

Muktasari:

  • Rais Samia Suluhu ameagiza korosho za msimu huu wa 2023/24 kusafirishwa kwa kutumia bandari ya Mtwara, akisema haoni sababu ya zao hilo kushindwa kusafirishwa kupitia bandari hiyo, huku akiagiza watakao tumia barabara kupata kibari toka kwa RC.

Mtwara. Rais Samia Suluhu ameagiza korosho za msimu huu wa 2023/24 kusafirishwa kwa kutumia bandari ya Mtwara, akisema haoni sababu ya zao hilo kushindwa kusafirishwa kupitia bandari hiyo.

Kauli hiyo ameitoa leo kwenye mkutano wa hadhara katika ziara yake ya siku nne ambayo aliianza kwa kuongea na wazee, kuzindua Hospitali ya Kanda ya Kusini, mradi wa chujio, barabara ya kilomita 50; huku akiagiza watakaotumia barabara watalazimika kupata kibali.

Kibali hicho kwa mujibu wa Rais Samia, ni kile kitakachotolewa na Mkuu wa Mkoa (RC).

Amesema hapo awali, kulikuwa na baadhi ya mambo yaliyokuwa yakizuia kutosafirishwa korosho kupitia bandari hiyo, ambayo ni pamoja na kutokuwepo kwa makasha, ambayo kwa mujibu wa Rais, makasha hayo sasa yapo.

"Mwaka jana tuliambiwa hakuna sababu msingi ya kwa nini korosho isisafirishwe kupitia bandari yetu... tunaambiwa makasha kuwa yapo zaidi ya 112 na bado yanaletwa, yanasubiri msimu uanze korosho iuzwe isafirishwe,” amesema Rais Samia na kuongeza;

“Lakini pia kuna wenye vituo vya mafuta, ambapo korosho ikitumia meli, hawafanyi bishara kwa maana ya malori kujaza mafuta... kuna mambo tofauti tofauti yanasababisha ukwamishaji wa bandari kutumika."

Rais Samia ameonesha hofu ya kutumia baraka katika usafirishaji wa zao hilo akisema: “Wanaposafirisha barabarani pia kuna uchakachuaji wa korosho ambao unaharibu sifa ya korosho zetu katika soko la dunia.”

“Nikwambie Mkuu wa Mkoa na Jeshi la Polisi, anaetaka kusafirisha kwa njia ya barabara lazima awe na kibali cha Mkuu wa Mkoa hadi gari itakayotumika nayo pia iwe na kibali na aeleze kwa nini anataka kusafirisha kwa njia ya barabara na zinaenda wapi,” amesema.

Rais amesema kwa kufanya hivyo, mkoa utapata takwimu sahihi za ujazo wa korosho, kule zilikotoka na kule zinakoelekea huku akitaka RC kuwatumia wakuu wa wilaya na kwamba kama hawawezi kazi basi ampelekee wengine.

“Hii bandari haikujengwa kuupamba Mkoa wa Mtwara, imejengwa ili kufungua mikoa ya kusini kupitia Mtwara, tunategemea itoe huduma kwa nchi jjirani, uchapakazi wenu ndio utavutia biashara zaidi,” amesema Rais Samia.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Plasduce Mbossa, amesema kuwa kazi kubwa imefanyika baada ya kujengwa gati mpya, ambapo bandari hiyo, imeanza kuhudumia shehena kwenda katika nchi za Comoro na Msumbiji.

“Bandari yetu inaweza kuhudumia mizigo mizito, tunayo mobile ‘scanner’ ambayo ina uwezo wa kufascan eneo hili, ili kuokoa mapato ya Serikali, pia katika eneo hili, tunao mtambo wa kupima mafuta sahihi ili kuweza kuokoa kodi zetu," amesema Mbossa.