Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yajitosa malori yaliyokwama mpakani wiki mbili

Arusha. Serikali imezuia shehena ya mahindi iliyokuwa ikisafirishwa kwenda nchini Kenya kupitia mpaka wa Namanga, baada ya kubainika baadhi ya wafanyabiashara kutokuwa na vibali vya usafirishaji mazao na usajili wa kufanya biashara hiyo.

Magari ya mizigo zaidi ya 100 kwa zaidi ya siku 10 yamezuiwa katika mpaka huo na kuibua malalamiko kutoka kwa madereva, wasafirishaji na mawakala wa biashara hiyo.

Hata hivyo, jana Mkuu wa Mkoa Arusha, John Mongella alisema tayari magari yaliyotimiza matakwa ya sheria yameanza kuruhusiwa kuendelea na safari.

"Kimsingi tumemaliza mgogoro, wafanyabiashara wanaotaka kupeleka mazao nje ya nchi wanapaswa kuwa na vibali na wenye navyo ndiyo watasafirisha mazao na tayari baadhi yao wamelipia na kuendelea na safari," alisema.

Akizungumzia mgogoro huo, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alisema chanzo cha mgogoro ni wafanyabiashara kushindwa kutimiza matakwa ya kisheria na taratibu za Serikali.

Alisema mfanyabiashara anayesafirisha mazao ya kilimo lazima awe na kibali ya kusafirisha mazao, namba ya mlipa kodi (TIN) na kampuni iliyosajiliwa.

Waziri Bashe, alisema baadhi ya wafanyabiashara hao hawajakamilisha mahitaji yanayotakiwa na ndiyo sababu ya mazao kuzuiwa kwa muda.

"Lazima mtu anayetoka nje ya nchi kuja kununua mazao Tanzania aheshimu utaratibu wa nchi, haiwezekani mtu kwenda hadi mashambani kununua mazao na kusafirisha bila kufuata sheria na hii hata kwa wafanyabishara wa ndani lazima waheshimu sheria," alisema.

"Hii itakuwa ni mara ya mwisho kuruhusu hali ya namna hii, wakati mwingine Serikali italazimika kutaifisha mahindi yanayosafirishwa kinyume cha sheria, kuna ambao vibali vimekwisha muda, wengine vibali vyao tayari vimesafirisha kiasi cha mahindi walichoomba hivyo wanapaswa kuomba tena," alisema.

Wasafirishaji

Wakizungumza na waandishi wa habari, baadhi ya madereva na wafanyabiashara, walisema wamezuiwa kuingiza mahindi nchini Kenya kutokana na sababu mbalimbali ambazo baadhi walikuwa hawana taarifa.

Mfanyabiashara wa Namanga, Paul Kivuyo, alisema hawajui sababu za kuzuiwa, kwani wanajua Serikali iliruhusu usafirishwa nje mazao ya wakulima bila vikwazo.

Dereva Thomas Urio alisema changamoto imetokea kutokana na kuzuiwa kuingiza Kenya mahindi ambayo wamekuwa wakisafirisha kutokana na kutolewa sababu mbalimbali ambazo awali wao kama madereva hawakujua.

"Nimekaa hapa leo siku ya tisa mahindi ambayo nasafirisha yameanza kuoza, kubadilika rangi, magunia mengine kuharibika hatujui hatima yetu," alisema.

Mwakilishi wa Chama cha wasafirishaji Tanzania, Zainabu Athuman alisema wametoa magari kusafirisha mahindi lakini baada ya kufika Namanga madereva wao wamezuiwa. "Sisi kama wasafirishaji, mwenye mahindi anakuja kwetu na kibali chake ndiyo tunatoa gari kusafirisha mzigo wake, sasa inapotokea shida sisi pia tunapata hasara," alisema.

Zainabu alisema magari yao kwa zaidi ya wiki mbili yamezuiwa Namanga na hakuna ufafanuzi kwa nini mahindi yamezuiwa kupelekwa nchi jirani na haijulikani kama baadhi ya wale wenye mahindi hawana vibali.

"Tunaiomba Serikali ifanye utaratibu kunusuru hasara ambayo inapatikana, kama kuna taratibu mpya basi zijulikane mapema ili kuzuia hasara kutokea, tunamuomba Waziri wa Kilimo na Waziri wa Uwekezaji watoe ufafanuzi," alisema.

Rais Samia aonya

Katika hatua nyingine, Rais Samia Suluhu Hassan pia amezungumzia suala hilo alipokuwa akifungua mkutano wa Baraza la Biashara (TBNC) jana jijini Dar es Salaam, ambapo alizungumzia changamoto za biashara kati ya nchi na nchi, akisema “nyingine tunaziunda sisi wenyewe ndani tunazipeleka nje.”

“Kwa mfano, atatoka dereva na lori lake la mahindi anakwenda nchi jirani, hana vibali vyote vilivyotakiwa kuwa navyo. Akifika mpakani hana kibali hiki kibali hiki, hana. Anakwama pale na anaanza mchakato upya lakini kelele mpakani tunazuiwa bila kusema huku ndani matatizo ni nini.

“Kwa hiyo tunapofanya biashara na wenzetu tuhakikishe tuna compliance ya hali ya juu ndani na kule tunakokwenda ili kuepusha haya,” alisema.