Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yakerwa mapigano ya wakulima, wafugaji

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini (wapili kulia) akisikiliza jambo kutoka kwa Mratibu wa Uhauwishaji wa Teknolojia na Mahusiano Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Naliendele Rashid Kidunda katika banda katika banda lao. Picha na Florence Sanawa

Muktasari:

  • Serikali hairidhishwi na imekemea migogoro ya wakulima na wafugaji inayooendelea nchini  katika baadhi ya mikoa ikiwemo Mkoa wa Lindi ambayo imetajwa kusababisha vifo.

Lindi. Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini amesema kuwa serikali hairidhishwi na migogoro ya wakulima na wafugaji inayoendelea kwa baadhi ya mikoa inayosababishwa na mahusiano hasi kati yao.

Akizungumza katika uzinduzi wa Maonyesho ya 30 ya Nanenane Kanda ya Kusini yanayofanyika katika Viwanja vya Ngongo mkoani Lindi, Sagini amesema kuwa Serikali inahuzunishwa kusikia wananchi wanapigana wanauana wakati  wanaweza kuishi kwa amani kwa kuzingatia matumizi bora ya ardhi.

“Mnatuambia kuwa hamkuwa na mifugo awali lakini leo mnayo mifugo tunatamani pia tule nyama, si ndiyo? Inahuzunisha kusikia wananchi wanapigana wanaumizana wakati wanaweza kuishi kwa amani haturidhishwi hali hii,” amesema.

“Katika siku za hivi karibuni imejitokeza migogoro baina ya wafugaji na wakulima katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Mkoa wa Lindi na habari mbaya sana imeelezwa hapa kuwa baadhi ya migogoro imetupeleka mpaka kwenye vifo, kama serikali hili haikubaliki,” amesema.

“Siyo sawa mfugaji awe kero kwa mkulima au mkulima awe kero kwa mfugaji natumia fursa hii kuwasihi wajiepushe na migogoro isiyokuwa ya lazima,” amesema.

“Tunafahamu wapo wasimamizi wa sheria hususani Jeshi la Polisi viongozi wa vijiji, kata na wilaya endeleeni kuwa imara katika kusimamia sheria ya mipango bora ya ardhi muwe imara katika kubaini mapema na kuchukua hatua stahiki wote wanaoonekana kuwa vinara wa migogoro kwa wakulima na wafugaji na kama maeneo yamepangiwa wafugaji basi wafugaji wakae kwenye maeneo yao na hawana sababu ya kuweka mifugo kwenye mazao ya wakulima,” amesema.

“Msimamo ulionyeshwa na mkuu wa mkoa wa Lindi  Zainab Telack wakudhibiti watu wa namna hiyo naomba uendelee kama hifadhi ama mashamba ya vijiji yamevamiwa tusikae kimya tuwe wakali,” amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack amesema kuwa mifugo imekuwa ikiongezeka kwa kasi ambapo wafugaji wengine wamekuwa wakiingia katika mkoa huo kinyume cha utaratibu.

“Wapo watu waliopoteza maisha na wapo waliopata ulemavu sababu ya migogoro ya wafugaji ambao wengine wanaingia kinyume na utaratibu tena wakiwa na makundi makubwa ya mifugo  na cha kusikitisha zaidi wanakuwa ndio chanzo Cha migogoro,” amesema Telack.

“Tumefanya Juhudi mbalimbali za kutoa elimu na hatua kali zinachukuliwa ili kuona mkulima na mfugaji wanaishi pamoja lakini kwa wale waliovamia hifadhi tunataka kuwatoa wote ili kuwawekea katika maeneo ambayo yamepangwa kwaajili ya mifugo,” amesema Telack.