Shahidi augua, kesi ya kina Mbowe yaahirishwa

Muktasari:

  • Kesi ya ugaidi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu imeshindwa kuendelea baada ya shahidi kulalamika kuumwa wakati akitoa ushahidi wake leo Jumatatu Januari 17, 2022.

Dar es Salaam.  Kesi ya ugaidi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu imeshindwa kuendelea baada ya shahidi kulalamika kuumwa wakati akitoa ushahidi wake leo Jumatatu Januari 17, 2022.

Shahidi huyo wa 10 wa upande wa mashtaka Mtaalamu wa uchunguzi wa uhalifu wa kimtandao wa jeshi la polisi, Innocent Ndowo alianza kutoa ushahidi wake asubuhi akiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Pius Hilla lakini ilipofika mchana alinyoosha mkono na kumueleza Jaji Joachim Tiganga anayesikiliza kesi hiyo kwamba anaumwa na hawezi kutoa sauti.

Kufuatia ombi hilo Jaji alijaribu kumshahuri shahidi apewe maji au avue barakoa aliyokuwa ameivaa.

Shahidi ananyoosha mkono juu

Shahidi: Samahani Mheshimiwa Jaji kichwa kinanigonga siwezi kuongeza sauti.

Jaji: Wakupe maji au unaweza kutoa hiyo barakoa

Shahidi: Hapana kutokana na kanuni za kiafya

Wakili Hilla:Tunajaribu kushauriana hapa shahidi ndio anajua mwenyewe

Jaji: Hamjawasiliana nae

Wakili Hilla: Shahidi anasema kichwa kinamgonga hayupo kwenye position ya kuendelea

Wakili Kibata. Shahidi mwenyewe ndio mwenye uwezo aseme kama tubreak kwa muda au tukirudi tuendelee au tuahirishe.

Wakili Hilla: Nilivyoongea nae kasema hayupo kwenye position ya kuendelea kwahiyo ngoja aseme mwenyewe.

Shahidi: Toka asubuhi nilivyokuja kichwa kilikuwa kinanigonga sasa kinazidi.

Jaji: Tukubaliane kugonga kwa kichwa ndio kuuma kwenyewe

Upande wa Jamuhuri sasa ia-address mahakama.

Wakili Hilla: Wakati Shahidi wa kumi akiendelea kutoa ushahidi wake hapa mahakamani aliieleza kuwa hajisikii vizuri hivyo hayuko kwenye nafasi ya kuendelea kutoa ushahidi.

Wakili Hilla: Na Shahidi anatakiwa wakati anatoa ushahidi anatakiwa awe na afya njema kwahiyo tunaomba shauri hili liahirishwe hadi pale afya yake itakapo imarika kwa kuwa hatujui atapona lini.

Jaji: Tunaye Askofu Mahakamani atakuombea na mimi nitakuombea shahidi Ili Kesho shahidi uweze Kuwa Mahakamani

Wakili Kibatala: Kwavile Shahidi amehojiwa aje kesho na kama atashindwa kuendelea na ushahidi wake basi kwavile sheria inaruhusu waje na Shahidi mwingine

Jaji: Naahirisha shauri hili hadi kesho kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa shahidi utakuja kwaajili ya kuendelea kutoa ushahidi upande wa mashtaka kama mtaona hali ya shahidi haijaimarika basi muandae Shahidi mwingine washtakiwa mtaendelea kuwa chini ya uangalizi wa Magereza.

Wakili wa Serikali Kidando: Mheshimiwa Jaji shauri linakuja kwa ajili ya kusikilizwa na tuna shahidi mmoja. Tuko tayati kuendelea.

Kibatala: Nasi tuko tayari kuendelea

Shahidi amefuatwa kwenye chumba cha waendesha mashtaka

Sasa shahidi anaingia na kupanda kizimba cha ushahidi.

Jaji: Majina yako

Shahidi: Naitwa Innocent Ndowo

Jaji: Umri wako

Shahidi: Miaka 36

Jaji: Kabila lako

Shahidi: Mchaga

Jaji: Dini yako

Shahidi: Mkristo

Wakili Kidando: Mheshimiwa Jaji Shahidi huyu ataongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi Pius Hilla

Shahidi anaaza kutoa ushahidi akiongozwa na Wakili Hilla….

Shahidi: Naitwa Inspekta Innocent Ndowo, kazi yangu ni afisa wa Polisi tangu 2012 kituo cha kazi Makao Makuu ya zamani

Shahidi: Nilifanya kazi katika kamisheni ya Tehama hadi 2014 nilipohamishiwa kamisheni ya forensic, Makao Makuu ya zamani ya Jeshi la Polisi.

Kamisheni ya uchunguzi wa kusayansi iko katika kitengo cha uchunguzi wa Makosa ya mtandao

Shahidi: Kitengo hicho cha cybercrime kinahusika na uchunguz wa vifaa vya kielektroniki ambavyo binahisiwa kuhusika katika makosa mbalimbali ya Uhalifu.

Shahidi: Katika Kitengo hicho mimi ni computer and mobile phone forensic analyst

Shahidi: Majukumu yangu ya msingi ni kupokea vielelezo toka Polisi vinavyohusika katika uhalifu na kufanya uchunguzi wa vielelezo kutokana na maombi ya taasisi husika

Shahidi: Jukumu lingine ni kuandaa ushahidi.

Shahidi: Jukumu lingine ni kuandaa ushahidi na kuuhifadhi

Shahidi: Lingine ni kuandaa ripoti ya uchunguzi

Shahidi: Taaluma niliyokuwa nayo mwaka 2009 niliipata katika chuo cha usimamizi wa Fedha na baadaye 2012 nilijiunga Polisi na 2014 Mei mpaka Juni nilifanya training certificate in ethical hacking katika chuo cha Unit Academy na baadaye Agosti 2014 kozi ya penetration testing  kutoka ATU

Shahidi: Mwaka 2015 nilienda India kwa kozi ya certificate course in networking chuo cha UPL Technologies Ltf

Shahidi: 2016 training nyingine Dar inaitwa Identification and Seizure of digital devices, chini ya Ubalozi wa Marekani.

Shahidi: 2016 nilifanya training ya Network Security Admistration na Kisha kozi nyingine ya terrorist crime scene investigation chini ya Ubalozi wa Marekani.

Shahidi: Baadaye Septemba 2016 nikwenda Egypt kwa kozi ya Criminal investigation and crime scene.

Shahidi: Novemba 2016 kozi ya digital forensic Laboratory mentorship program

Shahidi: Machi 2018 nilikwenda Rwanda kozi ya Cyber Crime Investigation.

Shahidi: Mei 2018 nilikwenda Uganda kwa koz ya Cyber Security

Shahidi: 2021 kozi ya Hacking katika Unit Academy.

Shahidi: Utaratibu wa upokeaji vielelezo huanza mapokezi ambako mchunguzi aliye zamu hukutana na afisa aliyetumwa kutoka taasisi huska akiwa na barua na vielelezo.

Shahidi: Jukumu la afisa wa zamu ni kukagua vielelezo na barua kujiridhisha usahihi wa vielelezo vilivyoletwa.

Shahidi: Barua lazima identify vielelezo husika.

Shahidi: Kama viko sawasawa afisa wazamu huvipa usajili wa maabara kwa kuandika detail zake kwenye Kitabu cha Kumbukumbu za maabara (Lab registration book) nauvipa namba kulingana na mwaka husika.

Shahidi: Hatua inayofuata ni kufungua jalada kwa madhumu ya kutunza kumbukumbu za vielelezo husika

Shahidi: Kisha vielelezo huska hutunzwa kwenye usalama na jalada linakwenda kwa commanding officer ambaye pia atalipeleka kwa Kamishna. Kisha litarudi kwa commanding officer ambaye ata- assign mtu ambaye atachukua vielelezo na kuviweka katika program ya uchunguzi

Shahidi: Uchunguzi wa vifaa hivyo vya kielektroniki hufanyika katika hatua tatu.

Shahidi: Kwanza ni acquisition (tuna-extract taarifa za kielekezo)

Shahidi: Ya pili ni analysis. Na ya tatu ni reporting.

Shahidi: Uchunguzi wa vifaa hivyo hufanyika kwa kutumia vifaa vya kimaabara.

Pia tunakuwa na forensic cable na data.

Shahidi: Hatua ya extraction hufanyika kwa kuunganisha vifaa husika kama ni simu inaunganishwa na mashine ya uchunguzi  kwa kutumia forensic cable ili kupata kilichomo ndani ya kifaa( kielelezo) mfano simu.

Shahidi: Mashine inapo-detect kifaa kwanza inakupa information kuhusiana na kifaa hicho, mfano simu namba, IMEI number. Baada ya. Ku-extract kilimo kwenye kielelezo kinapelekwa kwenye storage.

Shahidi: Hatua inayofuata baada ya extraction ni analysis ya extracted data ambayo inafanyika kwa kutumia mfumo uitwao Phidias analyzer ambao una kazi kuu tatu, kwanza decoding, advanced searching na ya tatu  ni reporting.

Shahidi: Decoding husaidia kuona files ambazo zisingeweza kuonekana.

Shahidi: Searching maana yake ni kutafuta kuona ujumbe unakusudia kulingana na terms of reference (hadidu rejea), ambazo hupatikana kwenye barua kuomba uchunguzi.

Shahidi: Madhumuni ya search ni kumsaidia mchunguzi maana kuna simu zinaweza kuwa na data nyingi, mfano simu inakuwa na GB kubwa sasa badala ya kusoma between lines, mfumo unakusaidia kupata kwa haraka kile unachotaka.

Advanced search ni kufanya in deep finding kwenye file ili kupata unachokihitaji

Shahidi: Reporting inafanyika baada ya kukamilisha hatua ya analysis. Reporting ni segment ndani ya mfumo wa physical analyzer, mchunguzi huweka pia matokeo ya uchunguzi, majina yake, namba ya kesi na  Lab number

Shahidi: Muda wote wa uchunguzi, mashine ina mfumo ambao ina access taarifa tu na hairuhusu manipulation na pia haitoa taarifa zote isipokuwa zile tu ambazo mpelelezi anazihitaji.

Shahidi: Zile taarifa zinazotoka kwenye vielelezo zinaweza kuwa printed au kuwekwa kwenye storage kutegeme na ukubwa wake.

Shahidi: Kwanza unafanya ulinganifu wa kilichoonekana kwenye mfumo kama ni halisi na wakati wote unatakiwa kuweka mark katika vielelezo, unaandika ripoti na kugonga mhuri wa nembo ya Polisi Bureau na kusaini kuonesha kwamba taarifa za kwenye document ni halisi.

Shahidi: Ripoti ninayoiandaa lazima iwe na findings nilizozipata, crime number, itaje vielelezo vyote, iwe na majina ya mchunguzi na kuhusiana na uchunguzi taarifa lazima ijibu zile hoja zilizoombwa na hata maelezo ya ziada.

Shahidi: Baada ya hapo nachukua vile vielelezo na kuvihifadhi, baadaye naziambatanisha na attachment nyingine na kuvihifadhi kwenye orodha kwa madhumuni ya kusubiri mpelelezi kuja kuchukua na pia kwa ajili ya usalama kuhakikisha kuwa hakuna mtu mwingine anaweza kuzichukua

Shahidi: Tarehe 13/8/2020, siku hiyo nilikuwa kituo changu cha kazi Maabara ya Uchunguzi wa Kisayansi katika Kitengo cha Uchunguzi Makosa ya Mtandao. Nilikuwa ofisa wa zamu mapokezi.

Shahidi: Siku hiyo moja ya kazi nilizopokea ni kutoka ofisi ya DCI (Ofisi ya Mkurugenzi Upelelezi Makosa ya Jinai) ilikuwa ni barua na simu nane.

Shahidi: Barua ilikuwa inaomba kufanya uchunguzi katika vile vielelezo na maombi yalikuwa yampita katika sehemu kuu tatu, kwanza ni kuangalia mawasiliano kupitia mitandao ya kijamii kama vile telegram, WhatsApp, Facebook, mawasiliano ya ujumbe mfupi wa maneno, miamala ya fedha, mawasiliano ya kupiga na kupigiwa, kati ya vielelezo vyote vile nane.

Shahidi: Pili, barua iliomba usajili (namba za simu hizo)

Shahidi: Tatu ilikuwa taarifa nyingine zozote zitakazosaidia katika upelelezi.

Shahidi: Baada ya kuvipokea nilikagua barua na vielelezo ili kuona kama viko sawasawa

Shahidi: Baada ya verification nili-assigne na kuandika kumbukumbu ya namba ya Maabara FB (Forensic Bureau/Cyber/2020/Lab/ 479.

Shahidi: Nilifungua jalada na commanding officer wangu alini-assign A/Insp. Innocent Ndowo kufanya hiyo kazi. Ni mimi wakati huo nilikuwa na cheo cha Assistant Inspector.

Shahidi: Taatifa za KYC za simu ambazo ziliombwa hazikuwa katika himaya yangu nililazimika kuziomba kwa watoa huduma wa mitandao miwili yaani Tigo na Airtel, ambako niliomba KYC na miamala ya fedha za namba za simu ambazo zilikuwa zimeambatanishwa katika ile barua ya maombi ya uchunguzi

Shahidi: Niliomba taarifa hizo tarehe Mosi, mwezi wa Saba, 2021, kuandika barua ya kiofisi kumbu namba CD/IR/27/2020, ambayo ni namba ya kesi( jalada). Lengo la kuandika namba hiyo ni kuonesha kwamba taarifa zinaombwa kwa sababu kuna kesi hiyo.

Shahidi: Nilipata majibu tarehe 2/72021.

Shahidi: Baada ya kupata taarifa hizo nilizisoma Kisha nilianza kufanya uchunguzi wa vile vielelezo ambavyo zilikuwa ni simu nane, Kama nilivyoeleza awali ( hatua za uchunguzi), baada ya kuzipa alama A mpaka H

Shahidi: Katika zile simu Tecno zilikuwa 4 Itel 2 Sumsang 1 simu moja

Shahidi: Kwenye analysis yangu simu ambazo zilikuwa na majibu ambayo ni positive zilikuwa ni nne na miongoni mwake kulikuwa na mawasiliano ya Mitandao ya kijamii ya WhatsApp na telegram, pia mawasiliano ya ujumbe wa maneno lakini pia katika taarifa za miamala ya fedha nilizoziomba kwa watoa huduma niliziona pia.

Shahidi: Kisha nilikwenda kwenye hatua ya reporting ambapo nili print taarifa za simu nne.

Shahidi: Baada ya kumaliza kuzi-print pia nilipata muda wa kuandaa taarifa yangu

Shahidi: Baada ya hapo nilivifunga vielele hivyo na kuweka alama majina yangu na nilivihifadhi, kusubiri mpelelezi kuja kuvichukua, lakini nilimkabidhi Inspekta Swila.

Shahidi: Nilimkabidhi zote nane, ripoti ya simu, ripoti yangu niliyoiandika, ripoti niliyoipata kutoka kwa watoa huduma za simu.

Shahidi: Baada ya kukabidhi niliendele na shughuli zangu binafsi.

Wakili Hilla: Mheshimiwa Jaji ni saa 7 kasoro dakika tano, hivyo nilikuwa naomba ahirisho kidogo tutaendelea baadaye.

Wakili Kibatala: Mheshimiwa Jaji hatujui kama bado ana maelezo marefu kiasi gani lakini tungemalizia tu hatua hii.

Kibatala anakwenda kwa kiongozi wa jopo la Waendesha mashtaka wanajadiliana kidogo Kisha anaijulisha mahakama kuwa wameomba mapumzika dakika 45 lakini naona bado upande wa mashtaka wanajadiliana.

Jaji Tiganga: Basi  tutakutana tena saa 7:45, naahirisha hadi muda huo.

Kesi imerejea baada ya mapumziko Wakili wa Serikali Mwandamizi Pius Hilla anaendelea kumuongoza Shahidi kutoa ushahidi.

Shahidi: Mashine inaponunuliwa utaratibu imewekwa kuna kuwa na namba za siri

Shahidi: Wakati wa kuomba taarifa kwenye mitandao ya simu niliandika barua na kuambatanisha na barua kutoka uchunguzi wa kisayansi.

Shahidi: Ripoti kutoka tigo nitaitambua kwa kuwa ina nembo ya tigo na sahihi ya mwanasheria.

Shahidi: Taarifa kutoka Airtel ina KYC na miamala ya fedha ya namba mbili ambapo zimeambatana na barua yenye nembo ya Airtel sahihi ya mwanasheria Glads Fimbari.

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama sasa nyaraka hizo zina namba zipi

Shahidi: Nyaraka niliyonayo hapa ni KYC pamoja na miamala ya fedha kutoka Airtel ina taarifa ya namba za simu ambayo niliomba. 0784779944, 0782237913 na 0787555200

Wakili wa Serikali: Namba hizo ulizitumia kuombea vitu gani?

Shahidi: Nliitumia kuomba KYC na miamala ya fedha.

Wakili wa Serikali: kwa Mujibu wa Taarifa ya Airtel, KYC holder ni akina nani?

Shahidi: Namba 0784779944 ilikuwa ina usajili wa Freeman Aikael Mbowe na namba 0782237913 ilikuwa ina usajili wa Halfan Bwire Hassan na namba 0787555200 ilikuwa na majina ya Denis Leo Urio.

Shahidi: Miamala niliyokuwa nimeomba ilikuwa ni kuanzia 1/6/2020 hadi tarehe 31/7/2020

Shahidi: Kwa mujibu wa uchunguzi nilisaini kulikuwa na transaction baadhi ya miamala ilifanyika tarehe 31/7/2020

Shahidi: 0784779944 ilituma fedha kwenda 0782237913 kiasi cha Sh80, 000….

Shahidi: Namba hizo ni sehemu ya namba ambazo zililetwa kwaajili kufanyiwa uchunguzi

Shahidi: Kwenye miamala ya tarehe 20/7,2020 kulikuwa na muamala kutoka 7801 900174 kwenda 0787555200 kiasi cha Sh 500,000 baada ya kufanyia uchunguzi nilweka kwenye taarifa zangu.

Shahidi: Taarifa nyingine ni KYC kutoka kampuni ya Tigo ambazo zinahusiana na namba 0719933386 kwa mujibu wa KYC inahusiana na Freeman Aikael Mbowe  

Shahidi: Tarehe 20/7,2020 kulikuwa na muamala wa Sh500,000 kutoka 25571933389 kwenda namba 25587555200 ambapo kwa mujibu wa taarifa ilikuwa ni miamala ya kuanzia tarehe 1/7,2020 hadi 2/7,2020

Shahidi: Kwenye Ripoti yangu niliambatanisha na simu nne ikiwemo tekno 2

Shahidi ananyoosha mkono juu

Shahidi: Samahani Mheshimiwa Jaji kichwa kinanigonga siwezi kuongeza sauti.

Jaji: Wakupe maji au unaweza kutoa hiyo barakoa

Shahidi: Hapana kutokana na kanuni za kiafya

Wakili Hilla:Tunajaribu kushauriana hapa shahidi ndio anajua mwenyewe

Jaji: Hamjawasiliana nae

Wakili Hilla: Shahidi anasema kichwa kinamgonga hayupo kwenye position ya kuendelea

Wakili Kibata. Shahidi mwenyewe ndio mwenye uwezo aseme kama tubreak kwa muda au tukirudi tuendelee au tuahirishe.

Wakili Hilla: Nilivyoongea nae kasema hayupo kwenye position ya kuendelea kwahiyo ngoja aseme mwenyewe.

Shahidi: Toka asubuhi nilivyokuja kichwa kilikuwa kinanigonga sasa kinazidi.

Jaji: Tukubaliane kugonga kwa kichwa ndio kuuma kwenyewe

Upande wa Jamuhuri sasa ia-address mahakama.

Wakili Hilla: Wakati Shahidi wa kumi akiendelea kutoa ushahidi wake hapa mahakamani aliieleza kuwa hajisikii vizuri hivyo hayuko kwenye nafasi ya kuendelea kutoa ushahidi.

Wakili Hilla: Na Shahidi anatakiwa wakati anatoa ushahidi anatakiwa awe na afya njema kwahiyo tunaomba shauri hili liahirishwe hadi pale afya yake itakapo imarika kwa kuwa hatujui atapona lini.

Jaji: Tunaye Askofu Mahakamani atakuombea na mimi nitakuombea shahidi Ili Kesho shahidi uweze Kuwa Mahakamani

Wakili Kibatala: Kwavile Shahidi amehojiwa aje kesho na kama atashindwa kuendelea na ushahidi wake basi kwavile sheria inaruhusu waje na Shahidi mwingine

Jaji: Naahirisha shauri hili hadi kesho kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa shahidi utakuja kwaajili ya kuendelea kutoa ushahidi upande wa mashtaka kama mtaona hali ya shahidi haijaimarika basi muandae Shahidi mwingine washtakiwa mtaendelea kuwa chini ya uangalizi wa Magereza.