Taarifa ya ubalozi kwa Watanzania waishio Ukraine

Muktasari:

  • Mashambulizi ya makombora ya Russia nchini Ukraine yameibua hofu raia wakiwemo Watanzania waishio nchini humo huku athari zaidi zikitarajiwa katika uchumi hapa nchini, hasa katika ongezeko la bei ya mafuta.


Dar es Salaam. Mashambulizi ya makombora ya Russia nchini Ukraine yameibua hofu raia wakiwemo Watanzania waishio nchini humo huku athari zaidi zikitarajiwa katika uchumi hapa nchini, hasa katika ongezeko la bei ya mafuta.

Jana, Rais wa Russia, Vladmir Putin aliagiza mashambulizi ya kijeshi mashambulizi ya mabomu nchini Ukraine kufuatia mzozo wa wiki kadhaa baina yao na jitihada za usuluhishi zilishindikana.

Taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden ambao unawakilisha pia Ukraine, uliwashauri Watanzania waishio huko kuondoka ikiwa wanadhani kubaki huko si muhimu kwa sasa.

Pia, ubalozi uliwataka wazazi wenye watoto wanaosoma nchini humo kufanya utaratibu binafsi wa kuwarudisha nyumbani kwa kutumia ndege za abiria zinazofanya safari kutokea Ukraine ili warejee nyumbani hadi hali itakapoimarika.

Soma zaidi: