TPB Bank na ajenda ya ujumuishaji kifedha

TPB Bank na ajenda ya ujumuishaji kifedha

Muktasari:

  • Watanzania wamekua pamoja na benki ya TPB na hivyo taasisi hii ina nafasi maalum katika akili zao. Ndio maana Watanzania wanaipenda sana na wanavutiwa na TPB Bank, ambayo serikali inamiliki sehemu kubwa.

Watanzania wamekua pamoja na benki ya TPB na hivyo taasisi hii ina nafasi maalum katika akili zao. Ndio maana Watanzania wanaipenda sana na wanavutiwa na TPB Bank, ambayo serikali inamiliki sehemu kubwa.

Januari mwaka 2017, benki hiyo ilibadili jina lake na nembo kutoka jina la awali la Benki ya Posta Tanzania  (Tanzania Postal Bank) na kuwa TPB Bank Plc. Hii ilifanyika ili kuendana na Sheria ya Benki na Taasisi za Kifedha ya mwaka 2006 ambayo ilitaka benki zote kusajiliwa chini ya Sheria ya Kampuni (Companies Act).

Mabadiliko hayo ya jina yalilazimisha pia mabadiliko ya nembo na kaulimbiu ili kuakisi mwonekano mpya. Ilianza kama Benki ya Akiba ya Posta ya Tanganyika (Tanganyika Post Office Savings Bank) mwaka 1925, hali inayoifanya kuwa moja ya benki za zamani Tanzania.

TPB ina matawi 84 (matawi kamili ni 48 na ambayo si kamili ni 36) ambayo yako katika kila mkoa wa Tanzania. Hii ni moja ya benki kubwa sana nchini na inaweza kuwafikia Watanzania wengi na kushiriki kukuza ujumuishaji wa kifedha.

TPB Bank Plc inatoa huduma zote zinazowafaa Watanzania. Huduma zetu za mikopo ni pamoja na Wastaafu Loan, ambao ni mkopo maalum kwa wastaafu wenye pensheni. Hapa tunashirikiana na mifuko ya hifadhi ya jamii na kukopesha fedha kwa wanachama wa taasisi zote za hifadhi ya jamii.

Pia tuna mikopo ya biashara, mikopo midogo, ya vikundi na wateja. Pia tunatoa huduma za kukusanya fedha taslimu kwa benki nyingine kama Citi Bank, Standard Chartered na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB). Tuna huduma ya kuhamisha fedha chini ya Western Union Money Transfer pamoja na kuchakata mishahara.

Kama uonavyo, tunatoa huduma za kifedha ambazo zinafaa kwa kampuni kubwa na mtu mmojammoja. Tutaendelea kuimarisha kujipanua kwa kufanya matawi yetu wakati wote kuwa ya kisasa na kufungua matawi madogo huku tukiegamia katika teknolojia.

TPB imechukua mikakati mingi katika maendeleo ya kiuchumi Tanzania. Mkabala (approach) wetu unaangalia watu ambao hawapati huduma za benki na ambao hata wakizipata, hazitoshelezi mahitaji na tunafanya haya chini ya utamaduni wetu wa kumjali mteja, uadilifu, ujumuishaji wa kifedha, unafuu na ubora.

Kwa kujiamini, tunasajili vikundi vya benki za kijamii vijijini (VICOBA) na kuviingiza katika mfumo rasmi wa kifedha na tunatarajia kushirikiana na taasisi zinazotoa mikopo midogo kwa ajili ya kuzikopesha. Kama benki, tumejiweka kama njia ya kukua kwa ujumuishaji wa kifedha ambao Watanzania wanataka ili kupiga hatua kiuchumi. Katika huduma za fedha kwa njia ya simu za mkononi, tumeshirikiana na M-PESA, Airtel Money, Tigo Pesa, Ezy Pesa na Halotel Money kuwezesha wateja wetu kupata huduma bora za fedha na benki kwa njia ya simu za mkononi.

Ushirika huu na waendeshaji wa huduma za simu za mkononi umezalisha M-KOBA, huduma ya makundi kuweka akiba, na Songesha, huduma ya kuchukua fedha inayozidi salio katika akaunti ya simu za mkononi.

TPB Bank inatoa huduma za uhamishaji fedha nje kwa kushirikiana na Western Union ili kuwezesha fedha kutumwa na Watanzania walioko nje kwenda kwa familia zao nchini Tanzania au kwenda kwa Watanzania walio nje.

Tunakubali kuwa malipo ya kodi yanasaidia kujenga sekta imara ya umma, kwa hiyo Watanzania wanaweza kufanya malipo Mamlaka ya Mapato  (TRA) katika tawi lolote la TPB Bank. Ili kukukabiliana na matukio yasiyotarajiwa, watu pia wanaweza kufanya malipo ya bima. Tunashughulikia miamala yote ya kifedha ambayo inanufaisha maendeleo ya kiuchumi Tanzania.

Wakati tukipanua huduma za benki kwa njia ya TPB POPOTE na mawakala, tunatoa fursa kwa biashara-- si tu kwa ajili ya kupanua mikondo yao ya mapato-- kujihusisha nasi, kupandisha hadhi za biashara zao na hivyo kukabili ushindani.

Hatua hizi zote zinasaidia kukuza utamaduni wa kuweka akiba na kusaidia Watanzania kujitengenezea maisha yao ya baadaye. Kama unavyoona, tunaenda sambamba na maendeleo ya kiuchumi ya Tanzania.

TPB Bank ni sehemu ya mtandao wa Umoja Switch, ambao una zaidi ya mashine 350 za kutolea fedha (ATM) wakati TPB Bank ina ATM 84 katika mtandao wake.

Tuna uwezo wa kuwafikia wateja wote ambao benki zao zinatumia mashine za Umoja, yaani NCBA na BOA hadi TPB Bank na Azania. Zaidi, kwa wateja wa M-PESA kuwa na uwezo wa kufanya miamala na ATM za Umoja, hili linapanua wigo wetu hadi kwa wateja watarajiwa.

Washindani wanaweza kutafuta maeneo yenye maslahi ya pamoja ili tufanye kazi pamoja kwa maelewano. Ushirika wa Umoja Switch unaonyesha kwamba hili linawezekana. Jambo muhimu ni kwa washindani kuangalia maeneo ya maelewano ya pamoja.

TPB imepania kuonyesha tofauti chanya ya mchango wake katika nchi kwa kuchangia baadhi ya faida yake katika jamii zenye matatizo.

Ikiwa moja ya taasisi za kifedha zinazooongoza katika kutoa huduma bora za kibenki nchini, TPB Bank ina jukumu la kuhakikisha shughuli zake za kuwajibika kwa jamii (CSR) zinakuwa fanisi na endelevu.

Maeneo yanayoangaliwa na mkakati wetu wa CSR ni matatu: elimu, afya na ustawi wa jamii.

Mikopo kwa wastaafu wa pensheni, ambayo inaitwa Wastaafu Loans, ni huduma inayotolewa kwa waliostaafu kazi ambao malipo yao ya pensheni yanatumika kama dhamana. Chini ya aina hii ya mikopo, mstaafu atapokea kiwango fulani cha fedha kinachowezwa kulipwa na kiinua mgongo chake au vyanzo vingine vya kuaminika vya fedha kama mapato yatokanayo na malipo kodi ya pango kukiwa na mkataba wa ukodishaji, biashara na mambo mengine.

Mikopo hii inahusisha wastaafu ambao ni wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo ni PSSF, HAZINA, NSSF na ZSSF.

Faida

 Hakuhitajiki dhamana ya mali inayoshikika

 Inasaidia wastaafu kuongeza mtaji kwa ajili ya miradi yao midogo na ya ukubwa wa kati

 Inawezesha wastaafu kupata fedha za mtaji kwa ajili ya kuanzisha biashara ndogo.

 Inatoa fedha kwa ajili ya wastaafu kukamilisha miradi yao

 Inawezesha wastaafu wenye pensheni kulipa ada za shule kwa watoto wao na wajukuu

 Inatoa fedha kwa wastaafu kwa ajili ya matibabu na mambo mengine binafsi

 Taratibu za kuchakata mikopo kwa wastaafu ni rahisi.

 Hatima ya maombi inatolewa ndani ya muda mfupi kadri inavyowezekana.

 Wastaafu wanafurahia nusu ya malipo yao ya kila mwezi

 Mkopo una bima ya kifo au ulemavu wa kudumu, kwa hiyo mzigo wa deni hafungi watu wengine katika familia yake.

TPB Popote Mobile Banking ni huduma ambayo inaruhusu wateja kufanya miamala ya fedha wakiwa mbali kwa kutumia simu za mkononi au vishikwambi.

Wateja wanaweza kufikia huduma hizo kwa kupiga namba *150*21# na baadaye kufuata maelekezo.

Huduma zinazotolewa na TPB Popote Mobile Banking ni pamoja na:

 Tarifa za miamala

 Maombi ya kujua salio kwenye akaunti

 Taarifa ndogo ya miamala kwenye akaunti (mini statement)

 Taarifa kamili ya miamala

 Kuhamisha fedha kutoka akaunti ya TPB kwenda benki nyingine

 Uwezo wa kubadili namba ya siri (PIN) mahali popote

 Kuhamisha fedha

 Malipo ya bili na tozo