TRA kukutana na wadau wa filamu Tanzania

Muktasari:

  • Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inatarajia kukutana na wadau wa filamu nchini Julai 10, 2021 katika ukumbi wa Chuo cha Kodi (ITA).

Dar es Salaam. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inatarajia kukutana na wadau wa filamu nchini Julai 10, 2021 katika ukumbi wa Chuo cha Kodi (ITA).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishna wa Kodi za Ndani, imeeleza kuwa watakutana kwaajili ya kujadili kodi mbalimbali zinazogusa mazao ya filamu ikiwemo kodi ya zuio na kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).

Imesema katika kikao hicho, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) itakuwepo kutoa ufafanuzi juu ya sera ya matangazo ya biashara kwenye chaneli ya kulipia.

“Aidha , Bodi ya filamu Tanzania ikiwa ni taasisi inayosimamia sekta ya filamu na michezo ya kuigiza nchini itahudhuria kama mlezi wa tasnia hiyo,” imesema taarifa hiyo.