Ukraine yalipua daraja kuzuia majeshi ya Russia kuingia Kyiv

Muktasari:

  • Wizara ya Ulinzi ya Ukraine imesema imelipua daraja la mto wa Teteriv liliopo kaskazini mwa mji wa Kyiv kwa jitihada za kuzuia wanajeshi wa Russia kuvamia eneo hilo.

Wizara ya Ulinzi ya Ukraine imesema imelipua daraja la mto wa Teteriv liliopo kaskazini mwa mji wa Kyiv kwa jitihada za kuzuia wanajeshi wa Russia kuvamia eneo hilo.

Katika taarifa yake wizara hiyo imesema wameweza kuzuia majeshi ya Russia kuendelea kuingia kwa kutumia mpaka wa Belarus uliopo umbali wa kilometa 32 kufikia mji mkuu.

Soma zaidi: Zaidi ya wanajeshi 40 wauawa Ukraine, mataifa yalaani

Karibu watu 18 na wanajeshi 40 wa Ukraine wameripotiwa kuuawa katika mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Russia leo Alhamisi Februari 24, 2022 asubuhi katika mji wa Odessa ulio pwani ya Black Sea, serikali imesema.

Taarifa zinasema zaidi ya wanajeshi 40 na raia 10 wamefariki katika saa za mwanzo za uvamizi huo, Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine aliwaambia waandishi.

Soma zaidi:Taarifa ya ubalozi kwa Watanzania waishio Ukraine