VIDEO: Sirro awaita ndugu wa Hamza kuchukua mwili

Sirro: Njooni mchukue mwili wa Hamza

Muktasari:

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, (IGP) Simon Sirro amewataka ndugu wa Hamza Mohammed aliyeuawa na polisi wakauchukue mwili huo kwakuwa wameshamaliza kuufanyia kazi.

Dar es Salam. Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, (IGP) Simon Sirro amewataka ndugu wa Hamza Mohammed aliyeuawa na polisi wakauchukue mwili huo kwakuwa wameshamaliza kuufanyia kazi.

Hamza aliuwawa Agosti 25, 2021 kwa kupigwa risasi na polisi dakika chache baada ya kuwauwa askari polisi watatu na mlinzi wa kampuni binafsi karibu na ubalozi wa Ufaransa na daraja la Salenda jijini Dar es Salaam.

IGP Sirro ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Agosti 28, 2021 wakati Jeshi la Polisi likiwaaga Makamishna wake, Balozi Valentino Mlowola na Robert Boaz amesema kuwa tayari wameshaufanyia kazi mwili huo hivyo ndugu zake wanaweza kwenda kuuchukua na wakishindwa mwili huo utazikwa na Halmashauri.


“Tunawakabidhi ndugu zake kwa sababu tayari sisi tumeshaufanyia kazi kama ndugu zake hawajaja kuuchukua waje wauchukue lakini siku zikifika na hawajaja kuuchukua Halmashauri itaenda kuzika”

Soma zaidi: Huyu hapa Hamza

“Hiyo familia ya Hamza inajisikiaje, fikiria wewe ungekuwa baba yake Hamza, mama yake Hamza, mdogo wake ungejisikiaje kuzaa kwako umetuletea balaa Watanzania, kwahiyo naomba Watanzania wengine wasituzalie watoto kama Hamza”