Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vyoo bora bado tatizo Tanzania

Muktasari:

Watanzania wametakiwa kuzingatia matumizi ya vyoo bora na kudhibiti majitaka na maji safi, ili kujikinga na maradhi yatokanayo uchafu wa mazingira.

Dar es Salaam. Wakati dunia ikiadhimisha siku ya choo, Watanzania wametakiwa kuzingatia matumizi ya vyoo bora na kudhibiti majitaka na maji safi, ili kujikinga na maradhi yatokanayo uchafu wa mazingira.

Siku hiyo inayoadhimishwa kimataifa kila ifikapo Novemba 19 ikiwa na kauli mbiu ya ‘Usafi na maji yatokayo ardhini, tufanye yasiyonekana kuonekana.’


Maadhimisho hayo yanakuja wakati Tanzania na hususani jiji la Dar es Salaam likikabiliwa na uhaba mkubwa wa maji na hivyo kuweka shakani usafi wa mazingira na upaikanaji wa huduma bora ya vyoo.


Taarifa zinaonyesha kuwa asilimia 33.5 ya makazi ya mijini kwa Tanzania Bara yana vyoo bora, huku vyoo bora kwa vijijini vikiwa ni asilimia 8.9, huku kati ya asilimia 70 hadi 80 ya wakazi wa ijini wakikosa miundombinu ya usafi vikiwemo vifaa vya kukusanyia taka.


Akizungumza kupitia taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu maadhimisho hayo jana Novemba 19, Mkuu wa shirika la Water Aid Tanzania, Anna Mzinga  amesema Tanzania inahitaji kuwa na ubunifu wa kitteknolojia ili kuwezesha wananchi kupata vyoo bora.


“Maji na usafi ni mambo mawili anayofuatana na hatuwezi kushughulika na moja bila kugusa la pili, hivyo ili kupata mazingira bora ya vyoo a kujikinga na maojwa yatokanayo na maji machafu, tunapaswa kutunza maji ya ardhini yasichafuliwe,” amesema.


Amesema kwa upande wao wamekuwa wakishirikiana na Serikali kujenga miundombinu ya kutibu majitaka na kutengeneza mbolea.
“Hii imesaidia wakazi wa Temeke kudhibiti majitaka katika msongamano wa watu na mifereji michache.


“Tunaiomba Serikali pamoja na wadau wa maji na usafi wa mazigira kutekeleza wajibu wao kwa kuangalia jamii za watu wasiojiweza kupata miundombinu ya maji na usafi inayokabiliana na mbadiliko ya tabia nchi,” amesema.


Kwa upande mwigine, utafiti uliofanywa na shirika hilo kwa kushirikiana na Wizara ya Afya mwaka 2021 kuhusu mazingira ya wafanya usafi katika sekta isiyo rasmi katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Arusha, imebainika kuwa wafanyakazi hao wapo katka haari ya kupata magonjwa.


“Kutokana na mazingira ya kazi yao ya sekta isiyo rasmi, wanafanya kazi chini ya kiwango na kutoa huduma hafifu.
“Serikali na wadau wanapaswa kuongeza uwekezaji katika seka ya usafi ili kila mwananchi apate maji safi na usafi wa mazingira,” imesema taarifa hiyo