Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wachimbaji wawili wapoteza maisha Geita, mwingine atumbukia shimo urefu mita 150

Muktasari:

  • Wachimbaji wawili wapoteza maisha huku wengine wanne wakijeruhiwa katika matukio mawili tofauti yaliyotokea wilayani Nyang’hwale mkoani Geita.

Geita. Wachimbaji wadogo wawili wamepoteza masiha na wengine wanne kujeruhiwa mkoani Geita katika matukio mawili toifauti likiwemo la imani Msalange (22) mkazi wa Kijiji cha Kayenze wilayani Geita kupoteza maisha baada ya kudondokewa na mwamba wakati akichimba dhahabu.

Tukio hilo limetokea Machi 29, 2023 saa nne asubuhi katika mgodi mdogo wa dhahabu uliopo kijiji cha shibalanga Kata ya Kaboha wilayani Nyanghwale mkoani hapa.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Berthaneema Mlay amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema mchimbaji huyo akiwa kwenye shughuli zake za uchimbaji aliangukiwa na mwamba ulililosababisha wachimbaji wengine Daniel John (27), Kibacha Ally (22) wakazi wa Kilimanjaro, Hassan juma (49) mkazi wa Babati Manyara na Sospeter Lugalila (38) mkazi wa Misungwi mkoani Mwanza kujeruhiwa.

“Hali ya mvua inayoendelea imesababisha mwamba kuwa dhaifu na ndicho kilichopelekea kuanguka na kuwangukia hawa wachimbaji ni vema wakachukua tahadhari hasa kwenye kipindi hiki cha mvua “alisema

Katika tukio jingine Sylivester Charles (29) mchimbaji mdogo wa dhahabu, mkazi wa Kijiji cha Shibalanga wilayani Nyang’hwale amepoteza maisha baada ya kuteleza na kudumbukia katika shimo lenye urefu wa mita 150.