Waliopigwa radi wakichimba kaburi Chunya wazikwa

Monday January 10 2022
Radi pc
By Mary Mwaisenye

Chunya. Miili ya watu wawili kati ya wanne waliofariki dunia kwa kupigwa radi wakati wakichimba kaburi imezikwa katika makaburi ya kata ya Kibaoni wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.

 Miili hiyo miwili ni kati ya minne ambayo iliyopigwa na radi Jumapili Januari 9, 2022 imezikwa leo.

SOMA: Radi yaua wanne wakichimba kaburi Chunya

Miili iliyozikwa leo ni ya Yohana James Ngosso na Swalehe Mbilinyi huku mwili wa  Boniface Lauleano ambaye ni mkazi wa Songwe ukisafirishwa kwenda  Itewe kata ya  Inyala Mbeya kwaajili ya mazishi.

Vilio na simanzi kwa wakazi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya vimetawala kutokana na tukio hilo kushtua watu wengi kutokana tukio hilo kutokea wakiwa wanachimba kaburi kwaajili ya kuuzika mwili wa mwanamke aliyefariki dunia Januari 07 2022.

Akizungumza katika mazishi hayo, Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mayeka S. Mayeka amewataka wakazi wa Chunya kuchukua tahadhari kwenye kipindi hiki cha masika ili kuepuka majanga.

Advertisement
Advertisement