Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanafunzi shule ya msingi wafanya upasuaji mfumo wa chakula

Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Chalinze Modern Seminary Wilayawakiendelea na kazi ya kumfanyia upasuaji mnyama aina ya sungura. Picha na Sanjito Msafiri

Muktasari:

  • Wanafunzi shule ya Msingi waanza upasuaji wa wanyama, watoa ushauri kwa Serikali baada ya mafanikio hayo.

Bagamoyo. Wanafunzi wa darasa la sita Shule ya Awali na Msingi Chalinze Modern Islamic Seminary wameiomba Serikali kutong’ang’ania mfumo wa utoaji wa elimu kwa vitendo kwa wanachuo pekee na badala yake utaratibu huo uanzie ngazi za shule za msingi hali itakayowezesha kuibua watalaamu wa kada mbalimbali ikiwemo madaktari na wauuguzi nchini.

Wametoa kauli hiyo Septemba 22, 2023 wakati wa maonyesho yaliyofanyika shuleni hapo, muda mfupi baada ya kufanikiwa kumfanyia upasuaji sungura ili kuangalia mfumo wa chakula kisha kumshona na mnyama huyo kuendelea na uhai wake.

“Huyu sungura ni wa sita tangu tulivyoanza kufanya upasuaji kama mlivyoona ujuzi huu tumeupata kupitia masomo ya nadharia na vitendo hapa shuleni hivyo tunaiomba serikali iondoe dhana kuwa baadhi ya masomo lazima yaanzie kidato cha sita hata yakianzia shule za msingi inawezekana’amesema Sajida Mohamed.

Amesema kuwa anaamini kuwa endapo serikali itaweka mfumo mzuri wa aina hiyo kutaondoa mkanganyiko wa baadhi ya wanafunzi ambao awali wanakuwa na vipaji maalumu lakini wanajikuta wanapotelea katikati wakiwa wakiendelea na masomo kwa ngazi mbalimbali hivyo kushindwa kutimiza ndoto zao.

Musa Swedi ameiomba Serikali kuongeza shule za vipaji maalumu kulingana na taaluma mbalimbali ili wanafunzi wawe wanapelekwa moja kwa moja kusoma huko kulingana na karama zao kuanzia ngazi ya awali, msingi na sekondari ili kuwapunguzia mzunguko mrefu wa kufikia ndoto walizonazo maishani.

Mwalimu wa masomo ya sayansi wa shule hiyo, Rashid Stambuli amesema kuwa mfumo wa masomo kwa vitendo unafaida nyngi kwa wnafunzi ikiwemo kuwapa ufahamu wa haraka huku ukiwapa msukumo wa kujielekeza kwenye vipaji vyao mapema.

“Huu utaratibu uko kwenye mataifa mengi kwenye nchi za wenzetu mwananfunzi anaanza kufundishwa kwa vitendo kuanzia ngazi ya chini kulingana na karama aliyonayo hivyo hata akifikia elimu ya sekondari tayari anakuwa ameiva sawasawa na kuwa mtaalamu mzuri anayeweza kujiajiri na hata kuajirika na akawa msaada mkubwa kwa jamii na Serikali kwa ujumla,” amesema.

Mkuu wa shule hiyo, Seif Hashimu amesemakuwa wakati serikali inaendelea na maboresho ya mitaala ya shule kuna umuhimu wa kukazia kipengere cha kuzingatia vipawa walivyonavyo wanafunzi ili kuwaanzishia kuanzia hatua za chini kwani kufanya hivyo Tanzania itaweza kuwa na wataalamu wa fani mbalimbali.