Wanafunzi Waafrika wabaguliwa Ukraine

Muktasari:

  • Wanafunzi Waafrika wanaosoma nchini Ukraine wamedai kuwa wanabaguliwa na vikosi vya usalama wanapokuwa katika harakati za kuikimbia nchi hiyo kuelekea nchini Poland.


Kyiv. Wanafunzi Waafrika wanaosoma nchini Ukraine wamedai kuwa wanabaguliwa na vikosi vya usalama wanapokuwa katika harakati za kuikimbia nchi hiyo kuelekea nchini Poland.

Mmoja wa wanafunzi hao wa Afrika aliyezungumza na shirika la habari la CNN, amesema yeye na wenzake walitakiwa kushuka katika usafiri wa umma katika kituo cha ukaguzi katika mpaka wa Ukraine na Poland.

Mwanafunzi huyo amesema waliambiwa wakae pembeni wakati basi linaondoka na raia wa Ukraine pekee yao.

“Zaidi ya mabasi 10 yalikuja na tulikuwa tukiangalia wakati wengine wakiondoka. Tulifikiria baada ya kuwachukua raia wa Ukraine watatupeleka sisi, lakini walituambia hapakuwa na mabasi mengi tena na tuliambiwa tutembee,” amesema.

China yaanza kuondoa raia wake Ukraine

Zaidi ya wanafunzi 400 waliopo mji wa Odessa na wengine 200 kutoka mji mkuu wa Kyiv wameondoka nchini Ukraine jana Jumatatu kutokana na vita inayoendelea nchini humo. Soma zaidi

Putin anataka nini Ukraine?

Kwa njia ya anga, nchi kavu na baharini, Alhamisi iliyopita Urusi ilianzisha mashambulizi dhidi ya Ukraine, nchi ambayo ni ya kidemokrasia ya Ulaya yenye watu milioni 44 na vikosi vyake viko viungani mwa mji mkuu wa Kyiv. Soma zaidi

Makombora ya Russia balaa nchini Ukraine

Uamuzi wa Rais wa Russia, Vladimir Putin kuanza mashambulizi ya angani na ardhini nchini Ukraine umezua balaa na kuwalazimu wananchi kukimbia maeneo yao kuokoa maisha. Soma zaidi