Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waziri apongezwa kuwa chanzo cha umaskini wa wavuvi

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (kushoto) na Naibu wake, Abdallah Ulega wakiwasikiliza wabunge waliokuwa wakichangia bungeni mjadala wa kupitisha  makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2018/2019, jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

Muktasari:

Aliyempongeza waziri huyo wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ni mbunge wa  Viti Maalumu (CCM), Agnes Marwa


Dodoma. Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Agnes Marwa amempongeza Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina  na watendaji wake kwa kuwasababisha umaskini uliokithiri wavuvi katika operesheni ya uvuvi haramu inayoendelea nchini.

Marwa ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Mei 17, 2018 katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi mwaka 2018/19 bungeni mjini Dodoma.

Amesema hiyo isipewe fedha za maendeleo kabisa kwa sababu fedha wanazokusanya zinatumika kuwapiga mabomu wavuvi.

“Waziri umeingizwa chaka na katibu mkuu na watendaji wake. Tuunde tume itakayokwenda kuangalia operesheni hii. Mheshimiwa  Rais haelewi yanayoendelea huko ziwani ni kama vile bomoabomoa wengine walijulikana kuwa  ameonewa,”amesema Marwa.

“Bunge hili liunde kamati kwa ajili ya uchunguzi kwasababu baadhi yao (wavuvi) wanachomewa nyumba, nyavu bila sababu ya msingi, wanaenda nje ya sheria wanavuka mipaka.”

Amesema anakubaliana na Mpina kuwa milipuko imepungua kwa wavuvi haramu lakini milipuko imeongezeka kwa watalaamu kuwapiga wavuvi wakati wa utekekezaji wa operesheni hiyo.

“Serikali ichukue hatua kuondoa mambo ya uonevu kama huwezi mwambie mheshimiwa Rais akuondoe, aniweke hata mimi niliyewahi kuwa mvuvi,”amesema Marwa.

Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema) Suzan Masele ameunga mkono kuundwa kwa tume maalumu ya kuchunguza  operesheni hiyo kwasababu haijafuata utaratibu wa kisheria.

“Wavuvi wanaombwa hadi rushwa Sh20 milioni,  wakikataa mnakamata nyavu zao na kwenda kuwachomea. Wavuvi wamekuwa wakionewa kwa kupewa adhabu ambazo hazipo hata katika Sheria ya Uvuvi ya Mwaka 2003 . Wengine wamekufa kwa presha,”amesema.