Wizara ya Habari kumshika mkono Miss Tanzania 2020

Saturday December 19 2020
wizarmisstanzaniapic
By Fortune Francis

Dar es Salaam. Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeahidi kutoa ushirikiano kwa mlimbwende wa Tanzania mwaka 2020, Rose Manfere ili aweze kuiwakilisha vyema nchi katika shindano la urembo la dunia.

Manfere anatarajia kushiriki shindano la Miss World mwaka 2021  baada ya Desemba 5, 2020 kushinda taji la Miss Tanzania.

Akizungumza leo Jumamosi Desemba 19, 2020 Waziri wa Habari, Innocent Bashungwa amesema wizara hiyo na waandaaji wa shindano la Miss Tanzania  kuna maeneo wanaweza kushirikiana.

"Tumekutana kumpongeza lakini tumeahidi kushirikiana na waandaaji ili akumbuke popote anapokwenda amebeba nembo ya Taifa," amesema  Bashungwa

Amesema yapo maeneo ambayo wanaweza kushirikiana kuitangaza nchi ikiwemo ikiwemo kwenye sekta ya utalii.

"Baada ya mashindano haya kukamilika, mashindano yanayofwata ni miss world hapa nchi ndio inashiriki nia na mkakati popote atakapoenda anautangaza utalii"amesema Bashungwa

Advertisement

Mkurugenzi wa miss Tanzania Basilla Mwanaukuzi amesema toka kuanzishwa kwa mashindano hayo serikali imekuwa ikishiriki na kuwezesha kupeperusha vyema bendera.

Amesema lengo la mashindano hayo ni kutoa fursa kwa mabinti wa kike kupitia sanaa na kuitangaza Tanzania hasa kwenye utalii.

"Hatua inayofwata nikupeperusha bendera bendera ya Tanzania kwenye mashindano ya Dunia huyu alieshinda tayari ni balozi kila atakapoenda ataitangaza Tanzania,"amesema Mwanukuzi

Advertisement