Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vijana watakiwa kujitokea kugombea uongozi CCM

Muktasari:

  • Vijana wameshauriwa kugombea nafasi za uongozi ndani ya CCM na kuwaepuka watu wanaowakatisha tamaa.

Mtwara. Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mtwara Vijijini, Nashiri Pontiya amewahamasisha vijana kujitokeza  kugombea nafasi za uongozi ndani ya chama hicho, badala ya kukubali kukatishwa tamaa.

Pontiya ametoa kauli  hiyo leo Desemba 9, 2023  katika sherehe za maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru wa Tanzania Bara, huku akiwaonya vijana kuacha kutumika kukashifu viongozi.

Amesema kuwa ni vema vijana wakafanya mambo yatakayowafanya  waaminike na kupewa nafasi mbalimbali za uongozi.

“Vijana tuwanie nafasi za uongozi ndani ya CCM, tuache woga tuwe na uthubutu. Wakati mwingine vijana wanakatishwa tamaa ili wasigombee.

“Hizi nafasi tukumbuke wapo waliokuwepo wakatoka na sisi tutatoka wataingia wengine,” amesema.

Naye Naibu Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, Sixmund Lungu amesema kuwa miaka 62 ya uhuru inatosha kuonyesha wapi waasisi wao walipoanzia na wao wako wapi.

“Katika maadhimisho haya ni sehemu ya kukumbushwa wapi tulipo na tunayaona mafakio huko tundako, tumeshuhudia maendeleo makubwa ambayo nchi yetu imepiga,” amesema Lungu.