Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watoto saba wafariki kwa kusukumana uwanjani Malawi

Malawi. Watoto saba wamefariki dunia kutokana na kusukumana wakati wakiingia  katika Uwanja wa Taifa wa Malawi kuangalia mechi ya Nyasa Big Bullet dhidi ya Silver Strickers jana Alhamisi.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji wa Uingereza (BBC), tukio hilo lilitokea mjini Lilongwe kwenye Uwanja wa Taifa wa Bingu  ambako watu kadhaa wameripotiwa kujeruhiwa.

Chanzo cha vifo hivyo imeelezwa kwamba ni kutokana na mashabiki waliokuwa wameingia kwenye mechi baina ya Nyasa Big Bullet dhidi ya Silver Strickers kugombea kuingia uwanjani ili kuwahi viti lililosababisha kuanza kusukumana.

Rais wan chi hiyo, Peter Muthalika alityuma salamu za rambirambi kwa waathirika na ndugu za marehemu kutokana na ajali hiyo ya uwanjani na kuahidi kwamba Serikali yake itatoa ushirikiano kwa familia hizo.

Taarifa zaidi zinaeleza kwamba uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 40,000 mageti yake yalicheleweshwa kufunguliwa kwa zaidi ya saa tatu jambo lililosababisha watu kusukumana baada ya kufunguliwa.

Kamanda wa Polisi nchini huyomo, Lexan Kachama alisema huenda idadiya watu waliokufa ikaongezek kutokana na kuwapo idadi kubwa ya majeruhi.