Fred Lowassa: Tumerejea nyumbani CCM

Fred Lowassa 

Muktasari:

Fred ambaye ni mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema yeye pamoja na familia nzima ya Lowassa wamerejea nyumbani akimaanisha Chama cha Mapinduzi (CCM)

Arusha. Mamia ya wakazi wa Arusha wamekusanyika uwanja mdogo wa Arusha kumsubiri Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ambaye amerejea Chama cha Mapinduzi (CCM).

Lowassa aliyetimkia Chadema akitokea CCM ambako alipitishwa kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, Mei mosi, 2019 alitangaza kurudi CCM na leo Jumamosi Mei 9, 2019 anarejea nyumbani kwake, Monduli mkoani Arusha.

Watu hao wakiwepo familia ya Lowassa, wakiongozwa na mtoto wake, Fred Lowassa wamesema wamerejea nyumbani CCM na Lowassa.

Fred ambaye naye alijiunga na Chadema baada ya baba yake kutimkia Chadema Julai 28, 2015, amesema familia yote ya Lowassa imerejea nyumbani CCM.

"Kama alivyosema mzee amerudi nyumbani na sisi kama familia tumerudi kumuunga mkono" amesema Fred leo Jumamosi Machi 9, 2019 jijini Arusha.

Amesema anajisikia vizuri kurudi nyumbani kuendelea kushirikiana na rafiki zake ambao aliwaacha CCM na ambao bado wapo Chadema.

Baadhi ya makada wa CCM, walieleza Lowassa amefanya jambo zuri kurejea CCM kwani ndicho chama alichokulia.

Jeremiah Peter na Wilbard Shoo wanampongeza Lowassa kurejea nyumbani CCM.

Endelea kufuatilia Mwananchi kujua kinachoendea