Kaburi la Malkia Elizabeth II hadharani

Picha ya kaburi alipozikwa Malkia Elizabeth II

Muktasari:

Kasri la Buckingham Palace limeonyesha kwa umma kwa mara ya kwanza picha ya kaburi alipozikwa Malkia Elizabeth II.

Kasri la Buckingham Palace limeonyesha kwa umma kwa mara ya kwanza picha ya kaburi alipozikwa Malkia Elizabeth II.

Mtawala huyo wa muda mrefu wa Uingereza aliyefariki Septemba 8, 2022 huko Scotland, alizikwa Septemba 19 mwaka huu katika Kanisa la King George VI Memorial Chapel huko St George's Chapel, Windsor Castle, walipizikwa pia wazazi wake na mumewe.

Jina la Elizabeth II limeandikwa sehemu ya juu ya kaburi hil na lile la baba yake George VI, mama Elizabeth na mumewe Philip.

Picha inaonyesha jiwe lililowekwa ndani ya sakafu ya kanisa na kuzungukwa na maua.

Elizabeth II alianza kuliongoza taifa hilo akiwa na miaka 25 tu mwaka 1952.

Hadi anafariki katika visiwa vya Balmoral nchini Scotland alikokuwa anapatiwa matibabu, Elizabeth II ameiongoza Uingereza kwa miongo saba.

Mwaka 2015, alikuwa kiongozi wa kwanza wa Uingereza aliyehudumu muda mrefu zaidi katika historia ya nchi hiyo, akivunja rekodi iliyowekwa na babu wa babu yake Malkia Victoria na ndiye aliyekuwa mkuu wa nchi mzee zaidi duniani.

Pia alivunja rekodi ya Malkia Victoria, bibi wa babu yake, aliyetawala kwa miaka 63

Mwanaye wa kwanza Charles aliyekuwa mfalme wa Wales ndio atakuwa mfalme wa taifa hilo, kulingana na tamaduni za nchi hiyo.

Utawala wake wa muda mrefu ulipitia changamoto mbalimbali ambazo mara kadhaa zilisababishwa na mabadiliko ya dunia ambayo iliilazimu Uingereza kutoka kwenye utawala wa kifalme uliojikita haswa kwenye masuala ya kivita hadi kuwa Taifa la kisasa la kitamaduni ambalo liliheshimu uongozi wa kimila lakini maamuzi mengi yakikabidhiwa mikononi mwa waziri mkuu ambaye alitokana na vyama vya siasa.