Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi yathibitisha kumshikilia Mbowe

Polisi yathibitusha kumshikilia Mbowe

Muktasari:

  • Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza imethibitisha kumshikilia Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kwa mahojiano.

Mwanza. Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza imethibitisha kumshikilia Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kwa mahojiano.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Ramadhani Ng'anzi amesema kiongozi huyo wa chama kikuu cha upinzani nchini alitiwa mbaroni alfajiri ya kuamkia jana Jumatano Julai 21 akiwa hoteli ya Kingdom mtaa wa Ghana alikokifikia.

"Baada ya kumkamata, wenzetu wa Dar es Salaam nao walitueleza kuwa wanamtafuta kwa makosa mengine anayodaiwa kuyafanya huko; hivyo tulimsafirisha kwenda Dar es Salaam anakoendelea kuhojiwa," amesema Kamanda Ng'anzi.

Amesema kiongozi huyo wa Chadema hivi sasa yuko kwenye mikono salama ya polisi Mkoa wa Dar es Salaam na atarejeshwa Mwanza baada ya mahojiano ili aunganishwe na wenzake 15 wanaoshikoliwa kuhusiana na kongamano la Katiba Mpya lililozuiwa na jeshi hilo jana.