Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shahidi aeleza kutowatambua watu kwenye CCTV kamera kesi ya Sabaya

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya (wa tatu kulia) akiwa na washtakiwa wenzake sita katika mahabusu ya jengo jipya la Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha jana, ambapo kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili inasikilizwa. Picha na Janeth Mushi

Muktasari:

  •  Shahidi wa nane katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita, Johnson Kisaka, ameieleza Mahakama kuwa hawezi kuwatambua na kuwaelezea watu wanaoonekana kwenye video za CCTV, alizowasilisha mahakamani hapo.

  

Arusha. Shahidi wa nane katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita, Johnson Kisaka, ameieleza Mahakama kuwa hawezi kuwatambua na kuwaelezea watu wanaoonekana kwenye video za CCTV, alizowasilisha mahakamani hapo.

Shahidi huyo wa Jamhuri ni Ofisa uchunguzi wa maabara ya uchunguzi wa kielektroniki kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Makao Makuu.

Alidai mahakamani hapo kuwa video hizo za Benki ya CRDB Arusha tawi la Kwa Mromboo za Januari 22, mwaka huu alizichukua Mei 31, mwaka huu.

Alitoa ushahidi huo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, alipohojiwa na Wakili wa utetezi, Mosses Mahuna, mbele ya Hakimu Mkazi, Patricia Kisinda anayesikiliza kesi hiyo.

Shahidi huyo alidai kuwa aliagizwa kwenda kufanya uchunguzi wa taarifa za video zilizorekodiwa kwa CCTV kamera kwenye benki hiyo na ampatie Ramadhan Juma (Ofisa Takukuru) kwa ajili ya uchunguzi na ndiye ataweza kuelezea zaidi juu ya wanaoonekana.

Alidai katika video hizo sita aliona watu wakiingia na kupata huduma za kifedha katika benki, lakini jukumu lake halikuwa kuchunguza watu wanaoonekana, bali kuchukua video hizo na kuandaa ripoti ya namna alivyozichukua na kuziwasilisha kwa mchunguzi pasipo kuingiliwa.

Soma zaidi katika gazeti la Mwananchi leo Novemba 3, 2021. Na endelea kusoma tovuti  na mitandao ya kijamii ya Mwananchi kupata habari zote kesi ya Sabaya inavyoendelea mkoani Arusha.