Wataalamu watoa somo matumizi sahihi ya kondomu

Muktasari:

Baadhi ya watu hufungua kondomu na kuruhusu oksijeni kuingia kisha kuitumia baadaye, hali ambayo huchangia kuendelea kwa maambukizi yanayozuiwa na kondomu.

Dar es Salaam. Wataalamu wa maabara wameshauri kuwa mipira ya kiume na kike maarufu (kondomu) ambayo imehifadhiwa kwenye hali ya baridi ndiyo bora kwa matumizi.

Kondomu zilizohifadhiwa kwenye mazingira ya joto linalozidi digrii 30, zimeelezwa hupungua ubora wake na kuleta matokeo hasi kwa mtumiaji, ikiwamo kupasuka na kusababisha mwingiliano wa majimaji wakati wa tendo.

Wataalamu wa uchunguzi wa ufanisi wa dawa na vifaa tiba kutoka maabara ya Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) iliyopo jijini Dar es Salaam, walisema hayo jana wakati wakiendesha mafunzo ya nadharia na vitendo kwa waandishi wa habari.

Kupata uundani wa habari hii, jipatie nakala yako ya Mwananchi leo Alhamisi Machi 04, 2021