Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Huyu ndiye Waziri Mramba

Huyu ndiye Waziri Mramba

Muktasari:

  • Waziri wa zamani, Basil Mramba amefariki dunia leo Jumanne Agosti 17, 2021 kwa ugonjwa wa Uviko-19.


Dar es Salaam. Waziri wa zamani, Basil Mramba amefariki dunia leo Jumanne Agosti 17, 2021 kwa ugonjwa wa Uviko-19.

Akiwa ni mmoja wa mawaziri waliowahi kufungwa kwa makosa waliyoyafanya wakati wakiwa kwenye nafasi zao za uongozi.

Mramba ambaye amewahi kufungwa miaka mitatu kwa matumizi mabaya ya madaraka  alizaliwa mwaka 1940 alijiunga na Chuo Kikuu cha Makerere kilichopo Uganda na kupata shahada ya kwanza na baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha City London kilichopo Uingereza na kupata  Shahada ya Uzamili katika Biashara.

Amefanya kazi Serikalini katika nyadhifa mbalimbali. Alichaguliwa kuwa mbunge wa Rombo kabla ya kuteuliwa kuwa waziri.

Mwaka 2006, Mramba aliteuliwa na Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, nafasi ambayo aliitumikia hadi mwaka 2008 ambapo alibaki kuwa mbunge wa kawaida.

Huyu ndiye Waziri Mramba

Julai 7, 2015, Mramba na Yona walihukumiwa kila mmoja kifungo cha miaka mitatu jela na kulipa faini ya Sh5 milioni baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya Sh11.5 bilioni.

Kesi yao ilitokana na makosa waliyofanya wakati Mramba akiwa Waziri wa Fedha na Yona akiwa Waziri wa Nishati na Madini.

Hata hivyo, Februari 6, 2016, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliwabadilishia adhabu viongozi hao wastaafu na kuwa kifungo cha nje wakiwa tayari wametumikia miezi saba gerezani.

Katika kutekeleza adhabu hiyo, viongozi hao walitakiwa kuripoti na kufanya usafi katika Hospitali ya Sinza – Palestina kila siku siku asubuhi kwa miezi tisa. Walitekeleza adhabu hiyo mpaka walipokamilisha Novemba 5, 2016.

Tangu walipomaliza adhabu hiyo, Mramba hakuonekana hadharani kama ilivyo kwa wastaafu wengine maarufu. Amekuwa kimya kwa kipindi kirefu mpaka alipofariki leo Agosti 17 katika hospitali ya Regency kutokana na maradhi ya Uviko-19.